Wednesday, May 9, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA AWAMU YA KWANZA YA MAANDALIZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI, MKOANI TABORA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa Ramani ya makazi itakayotumika na Makarani katika zoezi la kuhesabu Sensa ya watu na makazi, na kusikiliza maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sensa, Hajat Amina Said Mrisho, wakati Makamu alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Picha ya Ramani ya Tanzania, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Vincent Mugaya, baada ya kufunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, Mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuhakiki Ramani ya iliyoandaliwa kwa zoezi la kuhesabu Sensa ya watu linalotarajia kuanza Tarehe  26 Mwezi Agosti, mwaka huu, wakati alipokuwa akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya Sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012, mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Mkoani Tabora wakati akifunga Awamu ya kwanza ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu akiwasili kwenye uwanja wa chipukizi mkoani tabora kufunga awamu ya kwanza ya maandalizi ya  sensa ya watu na makazi iliyofanyika leo Mei 9, 2012 katika Uwanja wa Chipukizi mkoani Tabora. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: