Picha ya maktaba
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
10/05/2012
Makamu wa rais Dk. Mohamed Gharib Bilal amesema kwamba Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania(IoDT) itasaidia kuboresha utendaji kazi kwa wakurugenzi wa taaasisi na mashirika mbalimbali na kuboresha utawala bora .
Aidha amewataka wananachi kuiunga mkono taasisi hiyo kwa kuwa ni chombo muhimu cha kikachosaidia kutoa mafunzo kwa viongozi hao na kuwaunganisha ili kuboresha utawala bora.
Kauli hiyo ilitolewa na Dk. Bilal wakati akizindua taasisi hiyo leo (jana) kwenye hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dares Salaam.
“Taasisi hii itakuwa inawachukulia hatua baadhi ya wakurugenzi ambao hawatafuata maadili na kanuni za IoDT ,ikiwemo kubadilishna mwazo na kupata uzoefu,” alisema Dk. Bilal.
Naye Mwenye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania(IoDT), Pius Maneno alisema taasisi hiyo ina wanachama 19 ambao kila mmoja amechangia sh. milioni 10 kwa ajili ya uanzishaji.
Alisema lengo kuwa la taasisi hiyo ni kutoa mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo viongozi hao , kujenga mtandao na kuandaa mikutano mbalimbali.
Katika uzinduzi huo , Profesa Geoffrey Mmari kutoka Chuo Kikuu cha Tuamini(TUDARG) na Mwenyekiti wa African Life Assurance , Ibrahim Mohamed walitunikiwa cheti cha uanachama wa heshima.
No comments:
Post a Comment