Monday, May 7, 2012

WABUNGE WA CHADEMA WADAI KUTOKUBALIANA NA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


NA PAULINE KUYE -NJOMBE
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo hakijakubaliana na baraza la Mawaziri ambalo limeapishwa leo na Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.
 
katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mkoa mpya wa Njombe kwenye uwanja wa polisi Makambako uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge wa Iringa mjini Mheshiwa Peter Msigwa, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mbunge wa Mbozi Magharibi ambaye pia ni katibu wa CHADEMA Tanzania Mheshimiwa David Silinde,wamesema uteuzi huo mpya wa baraza la mawaziri uliofanywa mei 4 mwaka huu sio suluhisho la matatizo ya Watanzania.
 
 Kwa upande wake Silinde amesema kuwa, kinachotakiwa kifanyike ni kubadilisha mfumo mzima na wale wote ambao wametajwa kwamba ni wezi wa mali za umma waende jela na wafilisiwe na si kuachwa bure.
  
Naye Mchungaji Peter Msigwa amesema kuwa Chama cha mapinduzi ni ukoo mmoja, wote wanafanana kitabia, kwa kubadilisha Baraza la Mawaziri kutoka nafasi moja kwenda nyingine haiwezi kusaidia kutatua ubadhilifu wa mali ya umma kwani bado ukoo ni ule ule.
 
Katika ziara hiyo matawi matatu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo pamoja na ofisi moja ya kata ilizinduliwa, huku zaidi ya wanachama wapya 600 walijiunga na chama cha CHADEMA

No comments: