Tuesday, June 19, 2012

Mabingwa Watetezi Waingia Robo Fainali

Jesus Navas alikuwa ni mkombozi wa timu ya Uhispania, kupitia bao la dakika za mwishomwisho dhidi ya Croatia, na kuiwezesha nchi yake kufuzu kuingia robo fainali katika mashindano ya Euro 2012.

Ilielekea kana kwamba mabingwa watetezi Uhispania walikuwa wakicheza mechi hiyo ya Jumatatu usiku kwa wasiwasi.
Hata hivyo Jesus, ambaye ni mchezaji wa Seville ya Uhispania, aliweza kuupokea mpira uliopigwa kwa maarifa na Andres Iniesta, na zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kumalizika, kuiandikishia Uhispania bao, na kuwahuzunisha mashabiki wa Croatia. Bao hilo moja lilihakikisha Uhispania inaongoza kundi la C.

Uhispania walicheza karata yao vyema, kwani kwa kumtoa Fernando Torres na mahala pake kuingia Jesus Navas, ni mchezaji huyo wa zamu aliyeweza kufunga bao.

Sasa mabingwa watetezi wanasubiri kujua kama watakutana na England au Ufaransa katika timu nane ambazo zitasalia kucheza robo fainali.
Kutoka bbc swahil:   http://www.bbc.co.uk/swahili

No comments: