Ryama Ally.
Sameer Salim Nimbu.
STAA wa filamu Bongo, Ryama Ally, juzikati alijikuta akichafuka kufuatia prodyuza wa filamu ya ‘Kiapo Changu’, Sameer Salim Nimbu kuweka hadharani mambo aliyodai ni mabaya ya msanii huyo.
Akizungumza na Amani, Nimbu alifunguka kuwa, Riyama amemsababishia hasara kubwa kwa kukatiza kucheza kipande cha filamu hiyo.
Nimbu alimtaja mwanaume mmoja (jina linahifadhiwa) kuwa ndiye chanzo cha Ryama kukiuka masharti ya mkataba kwani alimtukana matusi ya nguoni prodyuza huyo na kumuondoa kambini msanii huyo akitumia usafiri wa pikipiki aina ya Bajaj.
Alisema kuwa kuvurunda kazi kwa Ryama kulianza pale alipotakiwa kulala kambini na wenzake pale Mtongani Kaburi Moja, jijini Dar ambapo staa huyo aligoma.
Nimbu anaendelea: “Ryama alisema hawezi kudhalilika kwa kulazwa na wasanii wachanga wakati yeye ni mkongwe, akataka atafutiwe gesti.
“Nikaja gundua kuwa kumbe sababu ya yeye (Ryama picha ndogo) kuomba hifadhi mbali na wenzake ni mwanaume. Alikuwa na bwana’ke kwani nilipompatia chumba gesti, akawa anakwenda kulala naye kila siku hivyo hakutaka wasanii wachanga waone mambo anayoyafanya.”
Akaongeza: “Siku hiyo kutokana na mambo mengi tulichelewa kwenda kumchukua kule gesti kumpeleka shooting, cha kushangaza sasa, mwanaume huyo alinipigia simu na kunitukana akidai nimewaweka sana pale gesti bila kuwatumia gari, nilimjibu sina mkataba na yeye bali mwanamke wake.”
Aidha, prodyuza huyo aliendelea kudai kuwa muda mfupi baadaye alikwenda kumchukua na gari akaambiwa ameshaondoka na Bajaj na mwanaume wake na tangu siku hiyo hakuonekana tena kuendelea kumalizia kurekodi sehemu yake.
“Kwa sababu hiyo, ina maana nifute kipande cha mwanzo cha Ryama ili acheze msanii mwingine, ndiyo maana nikasema amenitia hasara kubwa,” alisema.
Ryama alipopewa nafasi ya kujibu tuhuma zake kwa kupigiwa simu yake ya kiganjani, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilikuwa mshiriki kwenye filamu hiyo, lakini siku hiyo anayosema niliamka naumwa sana, jamaa yangu akampigia ili kumjulisha, akamjibu mbovu, ndiyo maana nilikasirika sana na kuondoka gesti kwenda hospitali.
“Kwa sababu hiyo, sikuona sababu ya kuendelea kushiriki filamu yake maana hakutoa ushirikiano kwangu.”

No comments:
Post a Comment