Monday, June 25, 2012

Tawi la Chadema Washington DC limepokea Mwanachama Mpya Ambae Pia Amezawadia Tawi Hilo Zawadi Ya Gari Ili Kufanikisha Shuhuli Za Chama Hicho



Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakimkabidhi rasmi Hussein Kauzel Msabaha kadi ya uwanachama.

              Hussein Kauzel Msabaha akiwa na kadi ya Chadema


               Daftari la Sera ya Chama  Cha Demokrasia CHADEMA


Hussein Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi


 Wanachama wa tawi la chadema Washington DC wakipata picha ya pamoja


Hussein Kauzel Msabaha akimkabidhi funguo za gari Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi.


Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi akionyesha funguo za gari ya aina ya Chevy Suburban walilokabidhiwa na Hussein Kauzel Msabaha

 
Gari ya aina ya Chevy Suburban walilozawadiwa  Chadema na Hussein Kauzel Msabaha
Siku ya Jumamosi Juni 23, 2012, Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC lapokea zawadi ya gari aina ya Chevy Suburban kutoka kwa Hussein Kauzel Msabaha, baada ya kukabidhiwa rasmi kadi ya uwanachama mpya wa chama hicho jijini Washington DC
kiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi Majimbo mengine ya Marekani.
Naye mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu kwenye kukijenga Chama.
Picha na Habari na Mdau SwahiliVilla

No comments: