Kuna dhana kongwe sana kati ya kabila la wahaya ya kuwaita wale wasiyo kabila lao Banyamahanga (Gentiles)au watu wa mataifa.ni dhana kama ile ya wayahudi walivyokuwa wakiwaona watu wengine.kuna wanaosema hii ni dhana ya kibaguzi,na kuna wanaosema zipo sababu za msingi za dhana hiyo.katika muendelezo wa dhana hiyo haikuwa rahisi mhaya kuoa au kuolewa na mnyamahanga (asiye mhaya) jambo ambalo hata leo bado lina nguvu vichwani mwa wahaya wengi.kama kuna wanaojua sababu za wahaya kuwa na dhana hiyo watueleze,au basi ni ubaguzi tu wa ndugu zetu hawa? Na kama ni kweli kuwa wale wasiyo wahaya kama wasukuma,wakurya nk ni watu wa mataifa.
Masala Kulangwa
No comments:
Post a Comment