Sunday, June 3, 2012

WAPIGA KURA JIMBO LA ISIMANI WAMPONGEZA MBUNGE WAO LUKUVI KWA KUTEKELEZA VEMA AHADI ZAKE


Mbunge wa jimbo la Isimani Mhe.Wiliam Lukuvi akionyesha kitabu kinachoonyesha jinsi anavyotekeleza ahadi zake kwa wananchi wake

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa Bw Mhapa (kushoto) akiwa na mwenyekiti wa Iciso Mzee Kisinini na Bw John Kiteve mmoja kati ya watoa mada katika midahalo hiyo
Mdahalo ukiendelea katika ukumbi wa Hima Isimani jana
 
Na  Francis Godwin Blog
WANANCHI wa jimbo la Isimani mkoani Iringa wamepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na mbunge wao Wiliam Lukuvi na kumtaka mbunge huyo kuwawabana watendaji wasio wasio wajibika kwa wananchi.

Wananchi hao walitoa pongezi hizo leo kwenye ukumbi wa Hima Isimani wakati mdahalo wa wazi Kati ya mbunge Lukuvi na wananchi ,mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia Tanzania na kuratibiwa na asasi ya ISICO mkoa wa Iringa.

Akizungunza kwa niaba ya wenzake Maneno Kalinga alisema kuwa mbunge Lukuvi ni mbunge pekee katika mkoa wa Iringa kwa kufanya kazi karibu na wananchi wake ikiwa ni pamoja na kushughulikia kero za wananchi wake .

No comments: