Aggre Morris wa kwanza kushoto, John Bocco wakimpongeza Viallli (wa pili kushoto) kufunga la kusawazisha
Kikosi kilichoanza Azam
Kikosi kilichoanza Simba
MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, leo walikuwa wanapambana vikali na mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC, katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Urafiki, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa moja usiku.
Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika uwanja wa Amaan, Zanzibar, lakini Simba na Azam waliomba ifanyike Dar es Salaam.
Timu hizo zitakutana ikiwa ni baada ya Azam kufungwa mabao 2-0, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo, Azam watataka kulipa kisasi, baada ya kupoteza mchezo huo, lakini Simba itaingia ikiwa na shauku ya kuendelea kuibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo.
Wakizungumza Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu na msemaji wa Azam, Patrick Kahemele, walisema sababu ya kuhamia Dar es Salaam zinatokana na Uwanja wa Amaan kuwa mbovu na hauna viwango.
“Uwanja kwa sasa hauna hadhi ya kucheza fainali, hivyo tumekubaliana mechi hii ichezwe kesho (leo) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,”
Viingilio katika mechi hiyo ni Sh 30,000 kwa VIP (A), VIP B - 20,000, VIP C - 15,000, huku viti vya Orange vikiwa Sh10,000, Bluu na Kijani ni Sh 5,000.
No comments:
Post a Comment