Mkuu wa Mkoa Akifungua Mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe afungua rasmi mafuzo ya wakufunzi wa sensa mkoani Kagera jana tarehe 17/07/2012 na kuwaasa wajumbe wa mafunzo hayo kuzingatia yote watakayofunzwa ili takwimu sahihi za sensa na makazi ziweze kupatikana kwa ajili ya maendweleo ya mkoa wa Kagera.
Akiongea na wajumbe hao amesema kazi ya kuandikisha na kujua idadi ya wakazi na makazi sio kazi ya kuletea mzaa kwani taifa limeingia gharama kubwa sana katika kugalamikia mafunzo hayo na kama haitoshi kujua idadi ya wakazi wa Tanzaniani njia mojawapo ya kuiwezesha selikari kupanga jinsi ya kuleta maendeleo katika jamii.
Mratibu wa sensa mkoa wa Kagera akimkaribisha Mkuu wa Mkoa katika ufunguzin huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Linas Night Club, alisema dhumuni kubwa la mafunzo hayo ni kuwafundisha wajumbe hao kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Kagera ili watakapoiva wawe wakufunzi wa makarani wa sensa kuanzia ngazi ya Tarafa.
Mkuu wa Mkoa katika hotuba yake aliwasistiza sana wajumbe wote ambao walitoka katika kila wilaya kuzingatia sana mafunzo hayo kwa kuhakikisha kila kitu watakachofunzwa wanakizingatia kwa umakini mkubwa ili kuwa na uelewa mkubwa wa kwenda kuwafundisha makarani kule kwenye tarafa.
Pia Mkuu wa Mkoa aliwaonya wakufunzi hao kutojihusisha na vitendo vya kubuni au kukadilia takwimu pale watakapokuwa wanakusanya takwimu kwani ni muhimu sana kupata tawimu sahihi zitakazosaidia katika kupanga maendeleo ya taifa zima kwa miaka kumi ijayo. Vile vile alisistiza sana kuwa taarifa zote za sensa ni siri na hakutakuwa na mtu ambaye atatoa taarifa za kaya au za mtu binafsi zitakazoulizwa wakati wa sensa.
Wito; Mkuu wa Mkoa pia alitoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa siku ya kuamkia tarehe 26/07/2012 kwa kila sehemu ya mwananchi atayokuwa amelala. Pia alitoa wito kwa Taasisi za dini, na Taaasisi mbalimbali zote mkoani Kagera kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kujitokeza na kuhesabiwa. Mhe. Massawe alitoa angalizo kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote atakaye jaribu kuvuruga zoezi la sensa, hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja.
Mafunzo hayo ya sensa Mkoani Kagera yanaendeshwa na wakufunzi kutoka ngazi ya Kitaifa, aidha mafunzo yanayotolewa ni juu ya kutambua maeneo ya sensa, namna ya kuuliza maswali, namna ya kujaza madodoso pia mafunzo hayo yanafanyika kwa nadharia na vitendo na mwisho wa mafunzo hayo wakufunzi watafanya mtihani wa kujaribiwa kuona kama wameiva.
Imetolewa na:
Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa,
No comments:
Post a Comment