Ndugu Willy Mutabuzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa GESAP E,S CO LTD na MKJ WAJASIRIAMALI KAGERA Aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya kuhitimu mafunzo ya ujasiriamali (katikati) kwenye hoteli ya Vatican Sinza Dar es salaam leo jion.Kulia ni ndg David Elias Sindila,mkufunzi wa sheria,na kushoto ni Dkt.Mahamud Bakari mkurugenzi wa MOD INTERGRATED AND AWARENESS,walioendesha mafunzo hayo
Baadhi ya umati wa washiriki waliokuwa wakihitimu mafunzo ya ujasiriamali
Mgeni rasmi ndg Willy Mutabuzi akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo
Wahitimu wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi
Mgeni rasmi ndg Willy Mutabuzi akizungumza baada ya kusikiliza risala ya wajasiriamali iliyokuwa ikitaja changamoto wanazokabiliana nazo.Ameahidi kuwasaidia pamoja na mamlaka husika kutatua baadhi ya kero hizo
Mgeni rasmi akiendelea kutoa hotuba yake huku akisikilizwa na wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali,alisisitiza umuhimu wa kuunda umoja au vikundi ili kurahisisha shughuli za uzalishaji na wasiogope kukopa benki kwani hata wafanya biashara wakubwa hutumia mikopo kuendesha biashara zao,bali muhimu ni nidhamu katika matumizi ya mikopo.
Bwana Deodatus Leo akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo.
Mgeni rasmi akiteta jambo na ndg Dkt.Mahamud Bakari wakati wa sherehe za kukabidhi vyeti wahitimu wa ujasiriamali maeneo ya Vatican hotel sinza leo jijini Dar es salaam
Mgeni rasmi akiondoka ukumbini baada ya majukumu ya dhima ya sherehe kukamilika
No comments:
Post a Comment