Friday, July 20, 2012

RAY AFUNGUKIA SKENDO YA KUUZA GARI

Vincent Kigosi ‘Ray’ ndani ya gari lake.
Na Erick Evarist
MSANII maarufu wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameifungukia skendo ya kwamba ameliuza gari lake aina ya Toyota Lexus kwa kueleza kuwa, huo ni uzushi, mkoko huo bado anaumiliki.
Akizungumza na Ijumaa, Ray alisema madai ya kwamba ‘amelila njaa’ gari lake yamemshangaza kwani hawezi kufanya hivyo na hata kama itatokea atafanya hivyo kwa malengo.
“Unajua wabongo watu wa ajabu sana, hata hivyo hao wanaosema nimeliuza gari langu kwani walinipa mkopo? Hivi hayo maneno wameyatoa wapi, hao ni wazushi wanaopenda kufuatilia maisha ya watu,” alisema Ray.

No comments: