Friday, July 20, 2012

Straika Yanga apangusa kiatu cha Niyonzima

Haruna Niyonzima ‘Niyo’.
Na Wilbert Molandi
STRAIKA mpya wa Yanga, Said Bahanuzi, alishindwa kuzuia hisia zake za shukrani kwa kiungo wake, Haruna Niyonzima ‘Niyo’ na kujikuta akipangusa kiatu yake.
Tukio hilo lilitokea wakati Yanga ilipocheza dhidi ya Wau Salaam ya Sudan Kusini, Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Bahanuzi alipangusa kiatu cha Niyonzima katika dakika ya 12 wakati mechi hiyo ikiendelea, baada ya kuunganisha krosi safi ya kiungo huyo.
Wakati wachezaji wenzao wakishangilia bao hilo, Bahanuzi alimfuata Niyonzima na kupiga magoti huku mguu wa kiungo huyo ukiwa kwenye paja lake la kushoto, kisha kuanza kupangusa uchafu uliopo kwenye kiatu hicho aina ya Nike chenye rangi ya kijani na nyeupe.

No comments: