Baadhi ya wafanyabiashara walioko ndani ya soko kuu la Bukoba ambao manispaa inataka kuwaondoa kupisha ujenzi wa soko jipya.
Uongozi wa m ji wa Bukoba umewapa nafasi ya kuchagua wapi watapenda kuhamishiwa biashara yao kwa kipindi cha miezi 18 ambayo ujenzi wa soku jipya utakuwa umekamilika.
Mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Mr.Kaputa amesema kuwa soko hili litakalojengwa ni kwa ajiri ya wafanyabihasha wa bukoba na sio vinginevyo.
Pia amewahakikishi kuwa kwa yeyote atakayekuwa na bihashara ndani ya soko hili la sasa nafasi yake itakuwepo sio kama maneno yanayopitapita kuwa soko hilo ni kwa ajiri ya wageni na watu wenye bihashara kubwa kubwa tu.
Pia ametaja maeneo ambayo yameteuliwa kwa ajili ya wafanyabihasha hao kuchagua eneo zuri la kufanyia bihashara yao kwa kipindi cha miezi kumi na nane kuwa ni JENGO YA CCM, VIWANJA VYA BUKOBA SEKONDARI VILIVOPO MAFUMBO, SOKO DOGO LA KASHAI PAMOJA NA SOKO LA NYAKANYASI.
Lakini amekataa wazo la kuamishia soko hilo katika UWANJA WA KAITABA kwa kusema kuwa pale panamilikiwa na wanachi wa bukoba pamoja na Shilikisho la mpira Tanzania TFF.
Eliud
Bukoba
No comments:
Post a Comment