Monday, September 3, 2012

CHADEMA Vs POLISI: Mwandishi wa Habari auwawa na 'Bomu' akishambuliwa na Polisi Iringa

 
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi, pichani - amefariki dunia kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.Habari zilizotufikia kutoka huko, zinadai kuwa Mwangosi, ambaye ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo.
 
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa  Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Watanzania wenzangu,nachukua fursa hii kuwajulisheni kuwa sisi viongozi wa UTPC,tunakichukulia kitendo hiki katika daraja ya aina yake na katu hatutanyamaza kama baadhi watu wanavyodhani.Hili ni shambulio la kwanza katika historia ya tasnia
ya habari Tanzania ambapo mwandishi wa habari anakufa mikononi mwa mwa maafisa wa umma,anauawa akiwa kazini.Sasa kwanza tumemtuma Rais wetu Kenneth Simbaya aende huko kulikotokea tukio hili na kufanya uchunguzi ambao utatupa picha kamili na ataileta taarifa hiyo kwenye kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa UTPC kitakachofanyika trh 5 sep.Kwenye kikao hicho tutatoa msimamo juu ya jambo hili.Kwa sasa nnawaomba Wastanzania wenzangu,waandishi wenzangu tutulie,lakini nawaambia Hamkani si shwari tena tena.
Wakatabahu,

Kazi ya FFU Tanzania

askari wa FFU mkoani Iringa wakiwa wametanda eneo la uwanja wa Mwembetogwa ambalo Chadema ilipanga kufanyia mkutano wake leo wa kitaifa
Mkuu wa FFU mkoa wa Iringa afande Mnunka akiwa eneo la uwanja wa Mwembetogwa kuzuia mkutano wa Chadema
Mfanyabiashara eneo hilo la Mwambetogwa akihamisha bidhaa zake kukwepa shari eneo hilo ambalo limetangazwa kuwa ni eneo la hatari na FFU: Picha na Francis Godwin Blog-Iringa
 

No comments: