RAIS wa Chama cha Soka nchini Zambia-FAZ, Kalusha Bwalya amethibitisha kuwa mabingwa wa Afrika watachuana katika mchezo dhidi ya Bafana Bafana katika Uwanja wa Soccer City
jijini Johannesburg Novemba 14 mwaka huu. Mchezo baina ya timu hizo
umekuwa ukijulikana muda mrefu lakini uwanja ambao ungetumika kwa ajili
ya mchezo ndio ulikuwa haujajulikana mpaka Bwalya alipothibisha katika
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter. Itakuwa ni mara ya tatu
kwa Bafana Bafana kuutumia uwanja huo ambao ulijengwa upya kwa ajili ya
michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ambapo mara ya kwanza kuutumia
uwanja huo waliifunga Colombia mabao 2-1 katika mchezo wa kujipiama
nguvu na baadae kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mexico katika mchezo wa
ufunguzi. Afrika Kusini imecheza na Zambia mara nyingi zaidi toka nchi
hiyo iliporuhusiwa kucheza michezo ya kimataifa mwaka 1992 ambapo
wamekutana mara 14 huku kila nchi ikishinda michezo minne na kutoa sare
michezo sita
No comments:
Post a Comment