Mwenyekiti wa Chama cha
Mapindunzi (CCM) na mkurugenzi wa Star International Jesca Msambatavangu ,
amewataka wanafunzi wanaomaliza masomo ya elimu ya juu kuanza kujiandaa na
maisha yao sasa pasipo kuwa tegemezi.
Akizungumza na wahitimu
wanaotarajiwa kupata shahada na stashada kutoka katika vitivo mbalimbali katika
chuo kikuu cha Tumaini Iringa katika kongamano lililofanyika chuoni hapo siku
moja kabla ya mahafali. Msambatavangu ameeleza kuhusu jinsi alivyoanza kazi ya
ujasiriamali mpaka alipofikia kwa sasa.
“Nawaomba vijana wa kike na
wakiume muelewe kuwa maisha yenu ya sasa
na baadae yanategemea sana jinsi ulivyojipanga na kutumia fursa mbalimbali
haswa kupitia elimu uliyoipata katika kujiendeleza kimaisha "alisema.
Msambatavangu alisema mahali
ilipofikia Tanzania kwa sasa kuhusiana na suala la ajira na kueleza kuwa pasipo
kutumia fursa mbalimbali zilizopo wengi watabakia kulalamika kuwa hamna ajira
na kufanya kuwepo kwa idadi kubwa ya wasomi ambao bado wapo katika umasikini
mkubwa.
Mwenyekiti huyo alisema ana
uhakika kama wanafunzi hao watatumia uwezo na maarifa waliyopata wakiwa chuoni
hapo kwa vitendo watafanikiwa sana na kuwa waajiri wakubwa wa wengine na kuweza
kupata maisha yaliyo bora. Na kueleza maisha bora hayaji hivihivi yamtaka kila
mmoja kutumia fursa mbalimbali zilizopo kujiendeleza.
Katika kongamano hilo baadhi
ya wanafunzi walifanya vizuri katika taaluma, michezo, nidhamu, uongozi bora na
utunzaji wa mazingira, utafiti zilitolewa.
katika kitivo cha Uandishi
wa habari waliofanya vizuri katika taaluma ni Elisha Magolanga, Bebi Kapenya na
Fadhili Makenjula, Utafiti Lauson Mgani, Michezo Stella Munishi na Makenjula na
Katika nidhamu Elisha Magolanga na Neema Malwala hao wakiwa ni baadhi katika
vitivo vya taaluma mbalimbali vitolewavyo chuoni hapo.
Aidha mshauri wa kitivo cha
Sayansi ya jamii na sanaa Profesa Seth Nyagava amewapongeza waliopata tuzo na
kuwasihi wawe mabalozi wazuri waendako na kudhihirisha ubora wao.
Pia amewasihi wahitimu wote
kuzingatia yale waliyojifunza wawapo kazini ili waweze kudumu kazini.
Mahafali ya 15 ya Chuo cha
Tumaini yanatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 27 Oktoba mwaka huu chuoni hapo.
No comments:
Post a Comment