Nasseb
Abdul maarufu Diamond na Lina Sanga
wakifurahia madhari ya Bonde la Ngorongoro lililopo kwenye Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro(NCAA), juzi ili kuhamasisha wananchi walipigie kura Bonde la
Ngorongoro lishinde katika maajabu saba ya Afrika.
********
Mahmoud Ahmad Arusha
Vijana
nchini wameshauriwa kuvipigia kura vivutio vitatu vya utalii
vilivoainishwa hapa Tanzania iliviweze kuingia kwenye shindano la
vivutio vya asili vya afrika kwani wao wananafasi ya kufanya hivyo kwa
kuwa wanatumia mtandao kwenye shughuli zao nyingi za kila siku.
Kauli
hiyo imetolewa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Abdull Naseeb
almaarufu Diamond na Linah Sanga kwa nyakati tofauti wakati
walipotembelea mbuga za wanyama za Ngorongoro mwishoni mwa wiki na
kutanabaisha kuwa watatumia nafasi yao kama wasanii kuwaomba vijana
wenzao kuvipigia kura vivutio hivyo ikiwemo mbuga ya
Serengeti,Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro.
Kwa
upande wake Diamond alisema kuwa alikuwa akiwaona wanyama hao kupitia
kwenye runinga lakini ameweza kuwaona kwa uhalisia hivyo na kubaliana
kuwa sasa tubebe uzalendo kuweza kuvitangaza vivutio vyetu mahala popote
ulimwenguni na kuwataka vijana na watanzania kuanza kupenda utamaduni
wa kutembelea mbuga zetu kwani mbona wageni kutoka nje ya nchi wamekuwa
wao wakitembelea vivutio hivyo sisi je alihoji Diamond.
Diamond
alisema kuwa Tanzania imejaaliwa kuwa na vivutio ambavyo ni nadra
kukuta sehemu nyingine duniani lakini sisi tumekuwa nyuma kuvitangaza na
kuvitembelea huku ni kuwa watumwa wa wenzetu na kuwataka vijana na
watanzania kwa ujumla kuweza kuweka uzalendo na kuacha kutizama kupitia
Runigani vipindi vya wanyama na kwenda kutembela mbuga zetu popote
zilipo hapa nchini.
Na
kwa upande wake msanii Linah Sanga alisema kuwa yeye alikuwa hajawahi
kuwaona kwa uhalisia Simba na wanyama wengine kwa ujumla lakini ameweza
kuona wanyama hao na pia ameweza kuona Create jinsi ilivyo akiacha
alivyoso ma shuleni kwa kweli ni madhari ya kuvutia na inafaa kuipigia
kura ili iweze kuwemo kweny maajabu saba ya Afrika.
Linah
alisema kuwa wao kama wasani watawaomba vijana wenzao popote hapa
nchini kutumia muda wao wa ziada kutembelea mbuga zetu ilikuweza
kuitangaza vivutio hivyo kwenye kaya zao ili nchi yetu iweze kupata pato
kupitia utalii wa ndani na kuwataka watanzania kuvipigia vivutio vyetu
ilikuweza kushinda na taifa kuweza kuingiza pato.
Nae
Dkt Fransic Mumba kaimu mhifadhi wa mamlaka ya Ngorongoro alisema kuwa
ni bahati kwa watanzania kupata nafasi ya vivutio hivyo vitatu ikwemo
Ngorongoro,Serengeti na Mlima Kilimanjaro kuweza kupigiwa kura iliviweze
kuingia kwenye maajabu saba ya Afrika na kuwataka watanzania kuvipigia
kura Vivutio hivyo.
Dkt.Mumba
alisema kuwa anawaomba vijana wengi kuvipigia kura vivutio hivyo kwa
kuwa wamekuwa mstari wa mbele kwenye matumizi ya mtandao hivyo wataweza
kupiga kura kwa urahisi huku akitanabaisha jinsi ya upigaji wa kura
hizo.
No comments:
Post a Comment