Sunday, October 14, 2012

AFYA YA MTOTO JULIANA YAZIDI KUTIA MATUMAINI ZAIDI, NA HAWA NDIO WAMECHANGIA SIKU TATU HIZI


Afya na mtoto yatima Juliana Mwinuka mkazi  wa  kijiji cha Mavanga wilaya ya Ludewa  mkoa mpya  wa Njombe ambaye amelazwa katika  Hospitali ya Taifa  ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa jitihada mbali mbali za mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kupitia  wadau na wamaria wema mbali mbali imezidi kwenda vema .

Hadi hivi  sasa mtoto Juliana ambaye alikuwa hawezi  kuongea wala  kula kwa  sasa anaongea na ameanza  kula vizuri pamoja na kutumia dawa kama kawaida jambo ambalo linatia matumaini makubwa na kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa mtoto  huyo kupona iwapo afya  yake itaendelea kwenda vema zaidi.
Hata  hivyo madaktari  wa Hospitali  hiyo ambao kiukweli  wamekuwa msaada mkubwa kwa mtoto  huyo kwa sasa wanataraji  kumfanyia matibabu ya  mdomo wake ambao umetoa nje baada ya  kuungua na kutofanya mazoezi mara kwa mara  zaidi  wadau na wasamari  wema kuendelea  kujitolea kwa sara na michango mbali mbali ili mtoto Juliana aweze  kuendelea  kupatiwa matibabu na kupona .
 
Hawa ni wadau  waliojitokeza kuchangia kwa siku tatu kuanzia jumatano hadi leo Jumamosi  ni pamoja na  msamaria mwema mdau wa mtandao huu  aliyeomba kutotajwa  jina lake hapa (Tsh 15,500),Daniel Moyo (Tsh 20,000),mwanafunzi wa chuo cha Tumaini Iringa Frida Mwenda (Tsh 10,000),Glory Kaaya (Tsh 5,000)Yona Uriyo(Tsh 10,000),Hery Mgina (Tsh 11,000)na Thea Mtau (Tsh30,000

Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu ,mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi

Pia mmiliki wa mtandao  huu anapenda  kuwashukuru wamiliki wa mitandao mbali mbali na kurasa za facebook na vituo vya radio mbali mbali ambao  wameendelea kuungana nasi katika  kutoa taarifa  za mtoto Juliana Mwinuka ambaye sisi wadau ni kama baba na mama yake

No comments: