Friday, October 12, 2012

WANAWAKE MKOANI MTWARA WAKABIDHIW​A SIMU NA PESA KUPITIA M PESA KWA AJILI YA LISHE

Akina mama wa kijiji cah Nanguruwe mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe wakijumuika na maofisa wa Vodacom kufurahia simu walizopatiwa zikiwa zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom kuwawezesha kupokea fedha za mradi kwa njia ya M-pesa.
Afisa Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi akimkabidhi simu ya mkononi mmoja wa wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe kupitia M-pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika juzi katika kijiji cah Nanguruwe mkoani Mtwara.
Afisa Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi,akionesha aina ya simu iliyowekewa fedha katika akaunti ya M-pesa zinazotolewa bila malipo kwa kwa akina mama wanaonyonyesha kuwawezesha kupokea fedha za kunulnuia chakula chenye lishe kupitia mradi  wa Lishe bora na salama wa shirika la mpango wa chakula duniani – WFP. Mradi huo umezinduliwa juzi katika kijiji cha Nanguruwe, Mkoani Mtwara.
Baadhi ya wanufaika wa mradi wa kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula chenye lishe akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya M-pesa atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo hutolewa bila malipo na  Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.

No comments: