Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa
uzinduzi wa ‘Education for All Global Report’ ya mwaka 2012
inayoandaliwa na UNESCO kila mwaka, ambapo pamoja mambo mengi
aliyoyazungumzia pia amesema tukiwa tumebakiwa na si zaidi ya miaka
mitatu kufikia mwaka 2015, michakato ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya
Millenia (MDGs) na Malengo ya ‘Elimu Kwa Wote’ (EFA) lazima
irekebishwe.
Ameongeza kuwa japo
Tanzania inakaribia kutimiza lengo namba 2 la MDGs la ‘Elimu ya Msingi
kwa Wote na lengo la Tatu la Usawa wa Kijinsia lakini bado ziko
changamoto, akitolea mfano katika elimu na kusema msisitizo umeelekezwa
katika kuongezwa kwa idadi ya watoto wanaojiunga shule lakini kimsingi
kinachotakiwa ni kuweka mkazo kwenye kiwango cha elimu kinachotolewa.
Mwakilishi wa Shirika
la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akiwasilisha matokeo ya ripoti
ya 10 ya ya mwaka 2012 ya ‘Education for All Global leo jijini Dar es
Salaam inayoitwa “Putting Education to Work” na kufafanua kuwa takriban
vijana milioni 2 nchini Tanzania hawajamaliza elimu ya msingi na hawana
maarifa ya kuwapatia kazi itakayowapatia kipato cha kujikimu kimaisha.
Amesema matokeo ya
ripoti hiyo yanaonyesha kuwa juhudi za haraka zinahitajika ili kuwekeza
katika kuwapatia vijana elimu haswa wenye miaka kati ya 15 hadi 24
Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taifa
Chama cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bw. Lwidiko Edward Mhamilawa
akizungumza katika uzinduzi huo na kuitaka Serikali kuangalia upya Sera
ya Elimu kwa kuwa haimwezeshi Mhitimu kuwa na uwezo wa kufanya kazi
itakayomwezesha kuendesha maisha yake na hivyo kuwa moja ya changamoto
kubwa inayoongeza idadi ya vijana wasiona ajira mtaani.
Kamishna wa Elimu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Eustella Bhalalusesa wakati
wa uzinduzi wa ripoti hiyo ambapo amesema Tanzania itaendelea kufanya
kazi bega kwa bega na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha
Sera za Elimu zinaboreshwa ili kuinua kiwango cha Elimu na kumjenga
kijana kuwa na stadi za kukabiliana na maisha hata kama hakufaulu
darasani.
Mwakilishi wa Shirika
la Kazi Duniani nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akisisitiza ili
kuboresha elimu walimu wanahitaji kupewa mafunzo bora, kupatiwa vifaa
vya kufundishia na mtaala wa Elimu kutoka ngazi ya Taifa mpaka ngazi za
chini unahitaji kufuatiliwa na kusimamiwa.
Moderator wakati wa
kuchangia maoni Juu ya Ripoti hiyo Profesa Idrissa Mshoro akitoa
tathmini yake kuhusiana na matokeo ya "Education For All Global
Monitoring Report" kabla ya kutoa nafasi kwa jopo la wataalam
waliohudhuria kuendelea na uchambuzi wao.
Jopo la Wadau wa
Kimataifa wa Elimu wakitathmini Ripoti ya UNESCO ya Mwaka 2012. Kutoka
kushoto ni Moderator Profesa Idrissa Mshoro, Deputy Head of Mission,
Head of Development Cooperation Division Ubalozi wa Sweden B. Maria Van
Berlekom, TVET Section Makao Makuu ya UNESCO Paris Bw. Borhene Chakroun,
Senior Technical Advisor, Education for Employment Bw. Peter Loan na
Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania Bw. Kabeho Solo.
Meneja Mipango wa
Ubalozi wa Shirika la Maendeleo la Itali katika Wizara ya Mambo ya Nje
ya Nchi hiyo katika Ubalozi wa Italia nchini Bw. Daniele Cristian
Passalacqua akichangia maoni juu wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo.
Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Bi. Vibeke
Jensen.
Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na Mwakilishi wa Shirika la Kazi
Duniani (ILO) nchini Tanzania Bw. Alexio Musindo.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka Mashirika ya Maendeleo, Mashirika ya Kijamii na Sekta Binafsi.
No comments:
Post a Comment