Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars ‘
wakiwasili jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam wakitokea nchini Uganda kushiriki michuano ya Cecafa Tusker Challenge iliyomalizika juzi. Kilimanjaro
Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
*******
Na mwandhishi wetu
Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars
iliyoshiriki katika mashindano ya Cecafa Challenge yaliyomalizika Jijini Kampala
Jumamosi, imerejea Jijini Dar es Salaam huku sasa ikitizamia kukutana na
Chipolopolo ya Zamzbia Disemba 23.
Stars, ambayo inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, ilirejea jana jioni kwa ndege ya Precision Air.
Kikosi hicho chenye wachezaji 18,
kilifanikiwa kutinga nafasi ya nne katika mashindano hayo baada ya kufungwa za
Zanzibar Heros kwa penalty 6-5 na kutinga nafasi ya tatu.
Katika mashindano hayo, The Cranes ya
Uganda ilifanikiwa kutetea taji na kubakiza kombe nyumbani. Hii nimara ya 13
kwa Uganda kutwaa taji hilo.
Akizungumza baada ya kurejea, Kocha Mkuu
wa Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen alisema mashindano haya yalikuwa muhimu sana
kwa timu yake kwani vijana wamepata uzoefu baada ya kukutana na timu ngumu na
zenye uzoefu.
“Mashindano yalikuwa mazuri…tulienda na
nia ya kurudi na kombe lakini hatujafanya jivyo ila muhimu ni kwamba mashindano
haya yametupa uzoefu mkubwa ili tuweze kujiandaa na mashindano mengine ambayo
yako mbele yetu,” alisema.
“Tumefarajika kucheza na timu kubwa kama
The Cranes ambayo ndio timu bora katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati,”
alisema.
Alisema sasa hivi macho ya wachezaji
yote yako katika mchezo ujao wa kirafiki dhidi ya Chipolopolo ya Zambia kwani
ni mechi ambayo itakuwa kipimo kikubwa kwa Stars kwa hivyo inahitaji maandalizi
makubwa sana.
“Nawaomba watanzania wasikate tama kwa
kuwa tunaijenga timu hawa ni vijana na ninaamini siku zijazo watafanya vizuri
zaidi,” alisema Poulsen.
Kocha Kim Poulsen anatarajiwa kutangaza
kikosi cha Stars kesho Jumatatu na amesema atawaita wachezaji wa Zanzibar pia
ambao walicheza vizuri Kampala.
“Niliwaona wakicheza kwa hivyo bila
shaka waliofanya vizuri watakuwemo kwenye kikosi hiki,” alisema.
No comments:
Post a Comment