Vifaa tiba vya macho, Wakazi Ruvuma wanufaika
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na International Center for Eye Care Education East Africa wametoa vifaa tiba vya Macho vyenye thamani ya Shilingi Milioni 3.5 mkoaniRuvuma.Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Huduma za Macho nchini Bernadetha Shiro alisema mpango wa Taifa ambao ulizinduliwa mwaka 2011 ambao utekelezwaji wake utafikia mwaka 2016 umelenga kutokomeza ugonjwa wa macho.
Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa huduma za macho nchini Bernadetha Shiro akiwa katika uzinduzi wa mwelekeo wa kituo cha tiba ya macho mkoani Ruvuma amesema wagonjwa wa macho wasioona kwa dunia nzima wapo milioni 30 na wagonjwa wenye uoni hafifu ni milioni 90.
Akitoa takwimu ya wagonjwa wasioona nchiniTanzaniaalisema ni wagonjwa 450,000 wenye uono hafifu kati ya wagonjwa 1,350,00.
Naye Mkuu wa Mipango kutoka Nchi za Afrika Mashariki yenye Makao yake makuu nchiniUgandaambaye anahusika na utoaji wa Elimu ya macho Dokta Naomi Nsubuga amesema shabaha ya ICEE (InternationalCenterfor Eye Care Education) ni kuhakikisha magonjwa yanayohusu macho yanatoweka kwa kufungua vituo Tanzania Bara na Visiwani.
Akipokea vifaa hivyo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dokta Ida Ngoi akishirikiana na Daktari wa macho Dokta Kyando waliwaomba wananchi wa Mkoa waRuvumakutokununua miwani ya mitaani ambayo itawaletea matatizo na kuongeza matatizo ya macho.
Mgeni rasmi kaimu katibu tawala mkoa wa Ruvuma Weston Nganiwa alieleza jinsi wananchi wanavyopata huduma ya macho katika hospitali ya mkoa waRuvuma.
Jumla ya wagonjwa 4918 waliwasili kupata tiba kwa ajili ya macho na kati ya wagonjwa hao 1080 walitibiwa wagonjwa 810 hawakuweza kufika hospitali ambao wana hitaji uangalizi wa karibu
Tanzania kama nchi nyingine zinazo endelea ina kabiliwa na upungufu wa watoaji wa huduma za macho,ikiwemo upungufu wa watalamu madakitari bingwa kwa asilimia na 80%upungufu wa vifaa tiba na madawa 75% pamoja na uelewa mdogo waelimu ya macho kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment