Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwa ndani ya treni asubuhi hii akiwapungia mkono WanaCCM
wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe
wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni
kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM
Msafara wa
Baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, ukiongozwa na Katibu Mkuu,
Abdulrahaman Kinana kuelekea Mkoani
Kigoma katika maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi umefika
salama Mkoani Kigoma na kupata Mapokezi makubwa kutoka kw2a wana CCM mkoani
hapo.
Msafara
huo ulio na Wajumbe hao wane wa Sekretarieti ya CCM, na wanahabari pamoja na
maofisa kadhaa wa Chama hicho ulizna safgari yake jijini Dar es Salaam Januari
25, 2013 majira ya saa 8:30 jioni na kusafiri usiku mzima njiani hadi kufika
Mjini Dodoma.
Wakiwa
njiani Usiku huo wajumbe hao walijumuika katika chakula katika Behewa maalum
linalotoa huduma hiyo ndani ya Treni hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akishuka katika treni Mjini Dodoma
Akisalimiana na Baadhi ya Wana CCM akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Wanachama
wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii
kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa
usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi
CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda
Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.Kushoto kwake ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na kulia kwake ni Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye
Wana CCM Mkoa wa Dodoma katika Mapokezi
Katibu Mkuu wa CCM aliingia katika behewa la Chakula na kujumuika na Wanahabari katika Chakula cha Usiku.
Blogger Father Kidevu akizungumza na Wajumbe hao wa Sekretarieti ya CCM
Muda ulienda na safari iliendelea
Maofisa wakiwa ndani ya Behewa
No comments:
Post a Comment