1. UTANGULIZI
“…meya atendelea kuwa huyo huyo…na mbunge ataendelea kuwa huyo huyo…kikao kinaagiza madiwani wote waliotia sahihi kusudio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na meya wamuandikie mkurugenzi kufuta kusudio hilo kuanzia kwa mbunge….kuungana na wapinzani kumtoa meya wa CCM ni usaliti kwa chama na adhabu yake ni ama kufukuzwa uanachama au kuwekwa chini ya uangalizi kwa miezi 48….kama munataka kurudisha kadi fanya haraka kabla hatujaendelea na kikao…” Kauli za Philip Manguka-M/mwenyekiti CCM TZ.
Kwa miezi kadha sasa siasa za Bukoba zimetawaliwa na malumbano ya Kagasheki (mbunge) kumtoa kwenye umeya Anathory Amani.
Vita ya wazi ilitangazwa rasmi na Kagasheki pale alipotaja kwenye mkutano wa hadhara kwamba “Amani nilimchonga mwenyewe…siwezi kumuogopa” mwezi November, 2012 katika uwanja wa UHURU PLATFORM.
Siku hiyo Kagasheki alimshambulia kwa nguvu kweli Amani, pamoja na kwamba siku hiyo hata Amani alikuwa pale jukwaani – kosa la kwanza kwa Kagasheki.Ajabu kila Kagasheki alivyoendelea kumtukana kuanzia uraia wake, uraia wa watoto wake, alivyomchonga n.k, Amani alibaki jukwaani huku akitabasamu, na mwisho alionekana jukwaani akicheza wimbo wa kumaliza mkutano wa kumshambulia. Nina uhakika kwa nje alikuwa anatabasamu na hata kucheza, lakini ndani alikuwa ana ghadhabu na kusononeka.
Ikumbukwe kwamba Kagasheki na Amani walikuwa bega kwa bega kupata ubunge wa Kagasheki, na mwishowe bega kwa bega kupata umeya wa Amani, na kwenye mkutano wa hadhara mwezi wa sita Kagasheki alimsifia Amani na kusema “..tumepata jembe…”.
2. NINI CHANZO CHA TATIZO?
Wataalam wa siasa za Bukoba wanasema tatizo la Amani na Kagasheki ni hulka zao wawili, wote wanapenda mafanikio yao binafsi, wote ni “timbigirwa” na wanafahamiana kwa karibu sana. Wakati Kagasheki anamsaidia Amani alitegemea mtu wa “waitu inya”, kumbe na Amani ana mawazo tofauti na “ambitions” tofauti. Mwisho wote walijikuta wanapenda ubunge wa Bukoba mjini. Kagasheki mara kwa mara amekuwa anasema hatogombea tena mwaka 2015, lakini kwa

hakika bado anataka kuendelea, au
hajawa na uhakika kama agombee au laa. Nae Amani anona kama huyo bwana
hagombei, basi ni zamu yake. Kwani Amani kwa muda mrefu anatamani kuwa mbunge.
Alijaribu Kataraia akamtemesha, akaenda Karagwe akapigwa, awamu hii ndo yuko
karibu na ubunge kuliko wakati wowote katika maisha yake.
Kama unataka kuona hasira ya Kagasheki, jaribu kuwa na mwelekeo wa kugombea ubunge Bukoba mjini!! Watu kadha wameishambulia vitisho, matusi, kejeli kwa kuhisiwa kuwa wanataka kugombea ubunge. Kwa kuanzia Mama Mushashu alijaribu kuanzisha ka SACCOSS ka wanawake, kakawa kanaanza kuwika na akina mama wakaanza kumsifia. (Ikumbukwe kwamba wanawake ndio ngome ya ushindi wa Kagasheki ukiunganisha na wizi wa kura) Mama huyo alishambuliwa kuanzia kwenye siku ya wanawake duniani kuanzia pale uwanja wa Kaitaba, kwenye mitaa na kila eneo mpaka akaamusha mikono. Akaja Mama Tibaijuka na Matrekta ya UN. Huyo alimtisha kabisa kwenye mkutano wa hadhara pale Rwamishenye, alisema wazi “..sitokubali, jimbo hili nimewekeza sana..”. kwakuwa yule mama ni mwanadiplomasia wala hakujibu akajiendea kwao Muleba akagombea na kushinda. Mwingine ni Karamagi na kiwanda chake cha MAJI ASILIA. Kagasheki ameishamtisha kwamba hataki mtu kuingilia jimbo lake, kama ni viwanda apeleke kwao Izimbya na pesa zake za kifisadi.
Kwa ufupi Kagasheki hataki kusikia mtu akizungumzia “jimbo lake”. Na washauri wake wake wanajua udhaifu wake huo, wakitaka kumuchuna ndio story ya kwanza.
Hata Amani, ndipo tatizo lilipo. Wakati wa kampeni Kagasheki aliahidi miradi mbalimbali likiwemo soko, lakini baada ya uchaguzi kama kawaida ya wanasiasa akajiendea Dar kwenye uwaziri. Amani akaanza kuchora namna ya kufika kwenye kilele. Si kwa pesa yake, ila kwa kutekeleza miradi aliyokuta manispaa. Alipiga hesabu nzuri kwamba akitekeleza miradi hiyo, kwanza itakuwa faida kwa wananchi, lakini sifa ya utekelezaji itampa nguvu ya kufikia ubunge bila mahangaiko makubwa. Wakati Kagasheki anasubiria Amani ampigie simu kwamba “waitu tugire tutai” Amani aliishaenda World Bank na NSSF kupata mikopo ya kuwezesha miradi yote kutekelezwa bila shida. Kagasheki hapo akajua amepigwa bao. Ilibidi aanze kuvunja mipango yote ya maendeleo bila kujali itakuwa na madhara gani kwa jamii na hata viongozi wenzake. Kwa ufupi ndio sababu ya msingi kwa nini ugomvi wa Kagasheki na Amani. Ubunge, ubunge, ubunge. Hapo Kagasheki anakufa na mtu!!! Sio kwamba unamsaidia kiuchumi au nini, ila anaupenda saaana, tena sana.
3. KAGASHEKI ALIKOSEA WAPI?
i) Hakuwa na sababu ya msingi
Kagasheki hakuwa na sababu ya msingi mbele ya watu ya kutaka kumtoa Amani. Sababu yake ya kweli kwamba anagangania ubunge asingeweza kuisema mbele za watu, hivo ikambidi kutumia pesa nyingi kumchafua Amani kuanzia pale Uhuru Platform. Maandalizi ya mkutano ule ilikuwa zaidi ya 5m bila usafiri wake wa ndege. Akawaendea madiwani kuwashawishi wamgeuke meya wao. Shida miradi ile yote aliyokuwa anapinga imepitishwa kwa vikao rasmi, watu wamesaini na kula posho. Waliokuwa wanalalamika kwamba wanaburuzwa wamechukuliwa picha za video tena na Jamal wakiwa wanapiga meza kwa furaha kubwa. Yeye mwenyewe wakati wa kampeni aliahidi kujenga soko, sasa wakati wa utekelezaji ndo anasema “water table iko juu” kwani wakati unaahidi water table ilikuwa chini sasa ndo imepanda!? Mwisho kwa kadiri alivyokuwa anendelea kujenga hoja ndipo watu wenye akili walikuwa wanaendelea kumuona sie. Kila mwenye uelewa mzuri amemdharau. Ametumia gharama kubwa kuwahonga madiwani wenye njaa kali mpaka akawapeleka Kampala wakaweka sahihi hoja ya kumtoa meya. Wakati wanaenda Kampala wameacha alama pote walipopita, sahihi zao mpakani zikachukuliwa, hotel walipofikia n.k na yote haya yamekuwa sababu za kushindwa kwake Kagasheki.
ii) Washauri wabovu
Kati ya mambo ambayo yataendelea kumtesa Mh.Kagasheki ni timu yake ya ushauri! Huwezi kuwa na Ashirafu Kalumuna kama katibu wako, Bingwa Jumanne msaidizi, Jamal (Jamco) na Mzee Kalumuna, Yusufu Ngaiza Kashai, ndugu zake Kagasheki family halafu ukafanya kitu cha maana. Wote hawa , ni watafutaji, wambea, wanafiki ambao wanataka kumhodhi Kagasheki kama mali yao binafsi. Wanamshauri ndivyo sivyo Wako tayari kumkosanisha na yeyote ilimradi wapate chochote.
Kuna wakati Kagasheki alikuwa na kamati ya maendeleo ya jimbo yenye watu wenye akili kama Mzee Rutabingwa, Fr. Mroso, Mzee Abdallah King na watu wa sampuli hiyo. Hawa ni watu ambao wanaweza kukueleza tena kwa nidhamu kwamba “waitu eki cheke”. Wakati anapambana na Amani amekosana na watu wenye busara kama Mkuu wa mkoa ambae ni mpenda maendeleo, mkuu wa wilaya, mkurugenzi n.k. Lakini yeye ushauri anautoa “seneti”. Sasa hao wanywa kahawa uwategemee kufanya maendeleo gani. Soko hili la Bukoba ndo kwanza wanaona la kimataifa, hawana vision. Hao ndo sampuli ya washauri wake. Angekuwa na watu wenye busara wangemuambia wewe simamia ujenzi wa soko ukamilike kabla ya uchaguzi utapata kura zako bila shida. Walikuwa wanamsahuri, mheshimiwa Amani ni kitu kidogo, tutamtoa, mpaka wakapanga meya mpya na makamu wake!
iii)Alimdharau Amani –Underestimate
Wakati anapiga hesabu zake hakujua uwezo wa Amani kisiasa, kifedha na uwezo wa kuhimili mikiki. Kwanza Amani ni mwanasiasa mzoefu na aliyekomaa kwa mbali sana kuliko Kagasheki, kwahiyo siasa za fitina Amani yuko mbali sana. Sijui kama Kagasheki anafahamu kwamba Amani amesomea siasa na baadae kupelekwa na CCM Israel kujifunza mbinu kali za kisiasa zikiwemo hata kubadili au tuseme kuiba kura. Kagasheki wakati anasema kumchonga Amani watu wenye uelewa walikuwa wanamshangaa. Amani amekuwa mwenyekiti vijana wa CCM mkoa kwa mihula 2, na baadae kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa. Huwezi kupenya CCM mpaka ngazi hiyo kama sio mwanasiasa halisi anayesubiri kuchongwa.
Amani ni miongoni mwa makada wachache wa CCM mkoani Kagera ambao wanatumika kwenye maeneo magumu yanayohitaji mbinu za kijasusi kufanikisha ushindi. K.m Kataraia alimtukana Amani kwenye uchaguzi na Rwakatale, alipigwa kura zaidi ya 1,700! Biharamulo Chadema ilikuwa imeweka mizizi kwenye Ubunge, Amani akaitwa na Mukasa akashinda, alipokuwa hapa anampigania Kagasheki kule Biharamulo Mukasa akapigwa.
Kagasheki mwenyewe anajua fika kwamba hapa Bukoba uchaguzi uliopita hakushinda kwa zaidi ya kura 5,000 kama inavyotajwa, Amani anajua na Kagasheki anajua kura zilipotoka, la muhimu kujua ni kwamba kura hizo hazikutoka kwa wapiga kura wa Bukoba wala Tanzania! Zilipotoka Amani anajua, na Kagasheki anajua kwa kuambiwa na Amani.
Kagasheki hakujua kwamba Amani hatishiki kirahisi. Sio mtu wa “kutishiwa nyau” kwa msemo wa vijana. Maisha yake mpaka alipo amepitia maisha ya karaha, mikopo, kujinyima, kukimbizana n.k. Wanaomfahamu Amani utajiri wake si zaidi ya miaka 15 iliyopita. Ameandamwa na visanga vya kitaifa kama urai, ameanza shule yake kwenye mazingira ya ajabu, ameanzisha ASECDO n.k. Kwahiyo maisha ya kupambana ni hulka yake, na mara nyingi anashinda. Kwa jeuri ya pesa ya Kagasheki angeomba msamaha yaishe, au angejihudhuru.
Kagasheki alijaribu kutumia kete ya urai, lakini akasahau kwamba imeishapitwa na wakati kwani tayari Amani ni raia kwa njia yoyote ile, labda aliwahada wananchi aliposema ndie alimsaidia Amani kupata urai wakati si kweli. Wakati Amani ana msukosuko wa uraia Kagasheki alikuwa bado nje ya nchi, hakuwa hata mbunge achia mbali uwaziri. Kataraia ndie alikuwa mbunge.
iv) Malezi ya Kagasheki
Inasemekana Kagasheki (MB) Muda mrefu hakulelewa hapa na hata lafudhi yake ni ya maeneo ya visiwani. Baba yao alikuwa mwenye msimamo mkali sana kwa watoto na alikuwa anataka wajitafutie mali yao binafsi sio kutegemea mali zake. Shuleni hakuwa na akili sana darasani lakini alikuwa mjanja na hodari wa mbio, hivyo akafanikiwa kupanda mpaka akajikuta ni balozi. Watu wa namna hii wakati mwingine hawashauliki. Wanajiamini kuliko kiasi. Wana jazba kutokana na kukataliwa na wazazi. Wakati viongozi wenzake wanamshauri achane na Amani yeye alikuwa hasikii. Malezi yake ndio yalikuwa yanamsukuma kulazimisha kitu ambacho hakina uwezekano wa kushinda.
v) Mbinu alizotumia
Katika mapambano yake, Kagasheki alitumia mbinu nyingi mbovu. K.m Kuwahonga madiwani kubadilisha maazimio ya vikao rasmi ilikuwa mbinu ya kijinga, kwani hata kama angefanikiwa kumtoa Amani, ingewalazimu kufanya upya mipango ya maendeleo kitu ambacho kingehitaji process ndefu kuanza kutekeleza. Mbinu hizi hazikujali maslai ya wananchi wa Bukoba na Kagera kwa ujumla. Amechelewesha au kukwamisha maendeleo ya jamii kwa ubinafsi wake.
Kitendo cha kwenda na madiwani Uganda wakiwemo na wa upinzani ilikuwa kosa la mwaka la kumfanya ashindwe vibaya sana. Cha ajabu yeye ndie alikuwa mtu wa mwisho kuweka sahihi kwenye karatasi ya kusudio la kutaka kumshinikiza meya wa CCM ajihudhuru, na kwa mantiki hiyo aliungana na vyama vya upinzani kuhujumu chama chake kitendo ambacho ni usaliti ndani ya chama. Kwa kusaini wa mwisho alidhihirisha wazi kwamba wote waliosaini wakiwemo wa CUF aliwaona na kuungana nao. Kwa kiwango cha Kagasheki alipaswa hili kulikwepa. Hili lilidhihirisha kwamba hafanyi kwa maslahi ya chama wala serikali, ila chuki binafsi dhidi ya Amani.
vi) Dharau kwa chama
Kagasheki kwa ndani anaamini yeye ndie mfalme na mhimili wa CCM Bukoba kutokana na pesa alizonazo. Katika vikao na viongozi wenzake wote walikuwa wanamuonesha kwamba anakosea, lakini yeye aliamini hawaelewi kitu. Yeye ni waziri, ataambiwaje na kamati ya siasa ya CCM wilaya? Wajinga tu hawa, nitazungumza na waziri mwenzangu, au raisi na yote yataisha. Amelewa madaraka na kusahau kwamba chama kiko juu ya watu wote. Viongozi wote wa chama tofauti na wale anaoweza kuhonga wote wakamchukia kwa kuwadharau. Madiwani akawaita mbumbumbu. Hivyo Mangula aliposhusha shoka asilimia 95% walishangilia kimoyomoyo au kwa uwazi. Wapambe wake aliokuwa amewahonga wakaishia mitini. Huwezi kusimama mbele ya wana”CCM na kuwaambia“..nilikutachama kimekufa..”, sasa wewe ulipitia wapi wakati chama hakikuwepo?
4- HITIMISHO
Kagasheki amekaa sana nje hivyo baadhi ya mambo ya kisiasa hapa hayajamkaa vizuri. Inabidi kuepuka jazba hasa wakati anazungumza mbele ya watu, kauli za“..Nilimchonga mwenyewe,” n.k hazifai kwa siasa za sasa hivi. Watu wanoleta maendeleo Bukoba sio wapinzani wako, nao wanachangia nyumbani kwao. Bukoba sio mali yako binafsi. Muhimu kuliko vyote unda kamati yako nzuri ya ushauri, kuna watu ambao ukiwa nao kama wapambe wako lazima watu wenye busara wakukimbie na mwisho itakuwa aibu kwako.
Kwa Amani, umeshinda hili lakini usidhani yameisha, unapaswa kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu ukijua kwamba kuna adui yako anakufata kwa karibu sana. Awamu hii hakuwa na udhibitisho wa tuhuma yoyote, kwa sasa anazitafuta. Jitahidi kufanya kazi kwa kufata taratibu zote kwani awamu hii umeokolewa na taratibu, na mwisho epuka kusema maneno mengi, kwani wanaokufurahia leo kesho usishangae ndio maadui zako kesho. Ndio maana kichwa cha habari kinasema “…JARIBIO LA KWANZA..”.Mengine yanakuja.
Mwisho wote tuungane kuleta maendeleo ya kweli Bukoba yetu, watoto wetu watatudharau sana tukiendelea kwenye mabishano ya kijinga. Kagasheki kwa hili amejishusha chini mpaka watu waliokuwa wanamuamini wanaanza kuwa na mashaka. Tuepuke oburushu, ihagiko, obunafu na mengine kama hayo.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI BUKOBA

No comments:
Post a Comment