Stori: Juddy Ngonyani
MAHAKAMA
ya Mwanzo mjini hapa, imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la
Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani,
kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000
mlalamikaji.
Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria
Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na
mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini
hapa.
Sista
huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa,
kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.
Katika
hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa
na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni ijulikanayo
kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24
mwaka jana majira ya saa 7 usiku ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya
Krismas.
Akisoma hukumu hiyo juzi, hakimu wa mahakama hiyo,
Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa
mzito wenye kuondoa shaka zote kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti
na utetezi uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.
Awali katika
utetezi wake mdaiwa aliiambia mahakama hiyo kuwa kwanza alikuwa
hajui kuwa Martin alikuwa mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo
kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.
Lakini Hakimu
Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku huo wa mkesha wa Krismas
mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na
mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu, walimkuta mdaiwa
na Martin wakitoka katika moja ya vyumba katika nyumba ya kulala
wageni ya Chipa, akasainishwa.
“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa
hana mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi
iliyoandaliwa na mwenyekiti huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh
700,000.
No comments:
Post a Comment