Saturday, February 16, 2013

MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA WA BINADMU ILOLO MBEYA

BARAKA KIBONA, MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU HAPA AKIWA NDANI YA GARI YA POLISI



MTUHUMIWA AKIPAKIWA NDANI YA GARI YA POLISI


HAYA MABOKSI INNASADIKIWA YALITAKIWA YAJAE HELA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA



BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA ILOLO WAKISHANGAA TUKIO HILO NYUMBANI ALIKOPANGA MTUHUMIWA HUYO



MNAMO TAREHE 12.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA NDANI YA NYUMBA YAKE .

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA KIUNGO HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA ANAKIRI KUMILIKI KIUNGO HICHO AMBACHO ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA KIENYEJI KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA NA FEDHA ZAKE.

TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO KWA BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO.

AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA KUUCHUKIA UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA UNAOJITOKEZA KATIKA MAENEO YAO.

Signed by
[B.N.MASAKI -SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MBEYA

No comments: