Kisawasawa Secondary School Headmaster in Morogoro, Menasi Msigwa receiving books donation from Dangio Kaniki Airtel Public relations and Event Officer second while from left looking on is Airtel Public relations and Event Officer Dangio Kaniki.
Airtel Public relations and Event officer Dangio Kaniki left challenging one of the students in Kisawasawa Secondary School during the book handover ceremony held at Kisawasawa Secondary school in Morogoro, behind left is Corporate Social and Responsibility Manager Hawa Bayuni, second left is Headmaster of Kisawasawa Secondary School Menasi Msigwa followed by Airtel Sales Officer Mohammed Mbamba.
Airtel Public Relations and Event Officer Dangio Kaniki (left) makinga point during the book handover ceremony in Kisawasawa Secondary School in Morogoro, left is the Corporate Social and Responsibility Manager Hawa Bayuni and right is the Headmaster of Kisawasawa Primary School Menasi Msigwa.
*****
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kupitia mpango wake wa 'Airtel shule yetu' imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule ya sekondari Kisawasawa ya mkoani Morogoro lengo likiwa ni kusaidiamaendeleo ya elimu mkoani hapo na kutoa huduma kwa jamii.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika shule ya sekondariKisawasawa na kuhudhuriwa na wawakilishi wa shule, wanafunzi,waandishi wa habari na wafanyakazi wa Airtel ambapo vitabu vyenyethamani ya shilingi milioni mbili vilikabidhiwa kwa shule hiyo.
Akiongea wakati wa halfa ya makabidhiano ya vitabu hivyo, Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki alisema, " Airtelinatambua kuwepo kwa uhaba wa vitabu na vifaa vya kufundishia katikashule zetu na katika kutatua changamoto hizo tunaongeza nguvu nakushirikiana na Serikali chini ya wizara ya elimu kuweza kuinua sektaya elimu.
"Tunafahamu umuhimu wa elimu katika kujikwamua na umaskini, hali ngumu ya maisha na kupata nguvu kazi ya kesho, kwa kutoa kipaumbele kwakusaidia na kuhakikisha nyenzo muhimu za kufandishia zinapatikana mashuleni ili kuweza kufikia dhamira yetu ya kusaidia jamii kwa ujumla Airtel inatoa fulsa sawa kwa shule zote nchini na leo tumewafikia wanafunzi wa Kisawasawa Kilombero Morogoro. Tunaamini elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunayo malengo ya dhati kabisa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Kisawasawa bw,Menasi Msigwa ameishukuru Airtel kwa kuwawezesha kupata vitendea kazi na kuongeza kuwa shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.
Aidha alichukua fulsa hiyo kuwaasa wanafunzi kutumia na kuvitunza vitabu hivyo ili viweze kusomwa na wanafunzi wengi zaidi na kuongeza kiwango cha kufaulu katika shule hiyo. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa msaada wa Vitabu kwa shule ya Mtipwa iliyopo mkoa wa Singida.
Tangu Airtel ilipoanza mpango wa kusaidia vitabu kwa shule mbali mbali za sekondari hapa nchini, takribani miaka saba iliyopita, imeshazifikia zaidi ya shule za sekondari tofauti zipatazo 1,000 nchini Hii ikiwa nikatika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.
No comments:
Post a Comment