Wednesday, March 13, 2013

HACHANA NA KIKAO CHA HARUSI CHAWIKI IJAYO HICHO KIWANGO CHA CHINI CHA HASNI ELFU MCHANGIE MTOTO HUYU

mtoto mwenye shida ya moyo aelekea muhimbili

Mtoto Simon Mlope akiwa na mama yake wakielekea Hospital ya mkoa wa Ruvuma , Na hii ni baada ya kutoa habari zake katika vyombo vya habari .

Mtoto Simon Mlope akiwa Hospital ya Mkoa wa ruvuma
Simon Mlope akiwa na mama (Amina Ally) yake Hospital ya Mkoa wa Ruvuma
 ..............................................................................
Mama wa mototo Simon Mlope (11) baada ya kupotelewa na matumaini ya kuokoa uhai wa mwanae anaesumbuliwa na ugonjwa wa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa  moyo wake una tundu hali ambayo inasababisha  kuvuta pumzi ,kula, kulala na kutembea kwa shida, nakumpelekea kushindwa kwendelea na masomo .

Sasa matumaini ya kuokoa uhai wa mwanae waanza kuonekana  nahii ni baada ya vyombo vya habari kutoa taarifa ya hali ya Mtoto SIMON MROPE kuzidi kuzorota kutokana na kukabiliwa na ugonjwa wa moyo unaohitaji matibabu nchini INDIA wasamaria wema wameanza kumchangia Mama wa Mtoto huyo akiwemo Mkuu Mkuu wa Mkoa wa RUVUMA SAID MWAMBUNGU ambaye amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa RUVUMA afanye taratibu za kumsafirisha mtoto huyo kutoka Mjini SONGEA kwenda jijini Dar es salaam kwa matibabu.

  Mama wa  Mtoto SIMON MROPE hawakua na hata pesa zinazowapa matumaini juu ya hatma ya uhai wa SIMON anayekabiliwa na maradhi ya moyo yaliyodumu kwa miaka 12 sasa mwilini mwake tena yakiambatana na maumivu makali.Watanzania wasamaria wema wameanza kumchangia fedha kupitia simu ya Mkononi, na wapo walioahidi kumchangia siku chache zijazo na pia kumtia nguvu na faraja,

Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo  anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE  ambaye ametelekeza familia yake  tangu mwaka 2011 hadi sasa hajulikani aliko , Awali aliondoka na kumuaga mke wake kuwa anakwenda kumjulia hali mama yake mzazi ambaye alipata taarifa kuwa ni mgonjwa kalazwa hospitali nchini Msumbiji. Nahii ni baada ya kuona hali ya mtoto si nzuri kiafya na inahitaji pesa kuweza kuokoa uhai wa mtoto simon, Baba huyu ambaye ni raia wa Nchi ya Msumbiji hadi hivi sasa hajulikani alipo kutokana na kukata mawasiliano na familia yake.

Kipato cha Mama huyu ni kipato cha chini sana ambacho hawezi kuendesha gurudumu la maisha  kulingana na hali yasasa na ukubwa wa familia yake. Mama huyu anafanya kazi za ndani na mwisho wa mwezi hulipwa fedha za kitanzania shilingi elfu thelathini(Tshs 30,000) na hapo alipo kapanga nyumba kwa mwezi analipa fedha ya kitanzania shilingi elfu kumi na tano( Tshs 15000) kwa mwezi.

Maisha ya mtoto huyu ni yashida sana kwani kula, kulala ,kuongea, kupumua na kutembea ni kwa shida sana, Maisha yake yamekuwa ni ya kitandani hata fraha ya maisha kwa sasa hana. Simon muda wote hubebwa mgongoni na hali inapokuwa mbaya zaidi humpelekea mama yake kushindwa kwenda kazini.Pia muda mwingi uladhimu kuwa karibu na mtu wa kumwangalia pale anapoenda kujisaidia haja kubwa na ndogo.
Kwa haya yote, Mama wa Mtoto SIMON MROPE akiwa na faraja ya mwanae kupata matibabu, anawashukuru watanzania wasamaria wema waliojitokeza na wanaendelea kujitokeza kumchangia kunusuru maisha ya mwanae,
Mwenye nia ya kuchangia matibabu ya Mtoto SIMON namba ya simu ya Mama yake ni 0752732290

No comments: