DR. JAKAYA KIKWETE AKIHANI MISIBA YA WALIOKUFA NA BOMU LILILOLIPUKA OLASITI JIJINI ARUSHA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke
wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu Regina Longino
Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika shambulio la kigaidi
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Jumapili iliyopita.
Mama Salma Kikwete akipungia
wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa
msichana Patricia Joachim Assey (10) katika kitongoji cha Majengo kata
ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita
katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji
cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke
wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim
Assey (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo
kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili
iliyopita Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia
ya Olasiti, jijini Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke
wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati
walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini
Arusha Askofu Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole
kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako pia alikutana na Maaskofu wa Makanisa
mbalimbali.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke
wake Mama Salma Kikwete wakitoa mkono wa pole kwa watawa wa kanisa hilo
wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa
Katoliki jijini Arusha Askofu Josephat Lebulu katika makazi yake
rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph, Parokia ya Olasiti ambako pia alikutana na Maaskofu wa Makanisa
mbalimbali. Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment