Friday, May 10, 2013

MHE. FREEMAN MBOWE AFIKA ARUSHA KUWAFARIJI WAFIWA NA WAHANGA WA BOMU LILILOLIPUKA OLASITI JIJINI ARUSHA

Mbowe addresses the media at Mt Meru
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ambae pia ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni Mh Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari jana jioni katika uwanja wa hospitali ya Mt Meru mara baada ya kutembelea kuwapa pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali hiyo kutokana na majeraha ya yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi-Olasiti lililotokea jumapili iliypoita.

Katika mazungumzo yake  Mh Mbowe aliwapa pole wote waliofikwa na janga hilo na kuwataka watanzania wote wawe watulivu huku vyombo vya dola vikifanya kazi yake lengo likiwa ni kuwapata wahusika na ijulikane hasa lengo lao kulipua bomu kanisani lilikuwa ni nini. Baada ya kutoka hopsitalini hapo Mbowe na msafara wake walielekea Elerai kuhani msiba mmojawapo.

Church members attention to Mbowe speechWaumini wa Kikatoliki wakimsikiliza Mh Mbowe (haonekani pichani) wakati alipofika kanisani hapo kuwapa pole.
Mbowe address the church peopleMh Mbowe akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Mt Joseph – Olasiti jana. Aliyemshikia kipaza sauti ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari.
Mhe. Mbowe akipewa maelekezo namna siku ya shambulio hali ilivyokuwa na Padri Festus Mangwangi wa Kanisa la Mt Josephat Mfanyakazi.Olasiti Arusha
Mbowe inside the churchMh. Mbowe akiwa ndani ya kanisa hilo
Padri Festus Mangwangi akitoa briefing ya tukio kwa MbowePadri Festus Mangwangi akielekeza mahali bomu lilipoangukia na namna watuwalivyojiokoa. Mbowe katika msafara wake aliambatana na wabunge wa chama hicho kwa majimbo ya Arusha Mjini na Arumeru Mashariki, pamoja na viongozi wa juu wa chama na Kanda ya Kaskazini.

Mbowe leave the churchMh Mbowe akiondoka eneo la kanisa mara baada ya kuzungumza na mapadri na waumini.
Mbowe na viongozi wengine wa chama na wabunge wakisubiri kuruhusiwa kuingia eneo la kanisa ambalo muda huo kulikuwa na ulinzi mkali kusubiri ujio wa Rais Kikwete
CDM people awaits Mbowe at Arusha AirportWafuasi na viongozi wa Chadema Arusha wakimsubiria Mwenyekiti wao Mbowe katika geti la wanaowasili uwanja mdogo wa ndege Arusha.

nassari lema wakimpokea mboweMbowe akiwasili uwanja mdogo wa ndege wa Arusha na kulakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Godbless Lema, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mhe. Joshua Nassari, Katibu wa Chadema Arusha na Kanda ya Kaskazini, Mh Amani Golugwa na Mwenyekiti wa Chadema Arusha Mh. Samson Mwigamba.
Chris Mbajo n others welcomes MboweChritopher Mbajo, wa Chadema Same anayefanya shughuli zake Arusha akimtambulisha Mh. Mbowe kwa makamanda waliokusanyika nje ya uwanja mdogo wa ndege wa Arusha kwa ajili ya kumpokea
Mbowe consoles Apolinary MalamshaMhe. Mbowe akimjulia hali Apolinary Malamsha aliyelazwa hospitali ya St Elizabeth. Hospitali hiyo ina majeruhi 20 na baadhi yao bado wana vyuma vya bomu mwilini.
Mbowe briefed by St Elizabeth doctorMbowe akizungumza na daktari wa hospitali ya St Elizabeth ya jijini Arusha
Mbowe consoles patient at Mt Meru hospitalMbowe akimjulia hali mtoto aliyejeruhiwa na bomu na kulazwa hospitali ya Mt Meru.
Mbowe St Elizabeth na mgonjwa Samwel PiusMbowe akimfariji majeruhi Samwel Pius aliyelazwa hospitali ya St Elizabeth
Mbowe at Mt MeruMjeruhi mwingine hopitali ya Mt Meru
Mbowe signs visitors book at St Elizabeth hospitalMh Mbowe akisaini kitabu cha wageni hospitali ya St Elizabeth
Women at Mt Meru grounds eager to gve hands to MboweMh Mbowe akizongwa na kina mama waliokuwa na shauku ya kumshika tu mkono alipozuru hopitali ya Mt Meru
Omar MatelephoneKamanda wa Chadema Jijini Arusha maarufu kama Omar Matelephone akiwa na wenzake uwanja wa ndege Arusha. Mh Mbowe alipokelewa na msafara wa magari 30 chini ya usimamizi wa Omary na mtu mwingine aliyetambulishwa kama Magoma Derick Magoma.

MKURUGENZI WA ULINZI WA CHADEMA BW. WILFRED LWAKATARE AFUTIWA MASHITAKA YA UGAIDI


MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemfutia mashitaka mawili ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare. 
Jaji aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.

Akizungumza na GPL, wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa.




  
Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.

Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.

Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao.

Ulinzi ndani ya mahakama.


Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.

Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.

Ulinzi nje ya jengo la mahakama.

Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.

Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake

Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki

No comments: