Saturday, July 13, 2013

BILIONEA ABRAMOVICH ATAKA AKADEMI YAKE, itoe WACHEZAJI KURITHI WAKONGWE

ambro 64b7a

Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Roman Abramovich (HM)
ambro2 49bdc
WAKATI Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich akitimiza miaka kumi ya umiliki wake darajani na kupondwa na baadhi ya makocha kwa sera yake ya kutumia fedha nyingi kununua wachezaji nje ya England na kuwanyima wazawa nafasi ya kucheza, sasa bilionea huyo mwenye kiburi cha pesa amesema anahitaji kuona maendeleo makubwa katika kituo cha kukulea vipaji cha klabu hiyo (Chelesea Academy) ili kuijenga upya timu yake.
Bilionea huyo anahitaji kuzalisha wachezaji wa kwake siku zijazo ili kuwarithi wakongwe wa wa klabu hiyo.
Wachezaji wakongwe wakiwemo nahodha John Terry na Frank Lampard – ambao walisainishwa mwaka 2001 kutoka West Ham, mpaka sasa wanaonekana kuwa ni moyo na roho ya klabu, hivyo Abramovicha amedai anatakiwa kuzalisha wachezaji wapya kutoka katika Akademi yake na kuachana na hasara kubwa aipatayo kwa kununua wachezaji wa bei kubwa. Chanzo: Sportmail

No comments: