Na:Lorietha Laurence-Maelezo
Taasisi
huru isiyo ya kiserikali kutoka nchini Marekani inayoitwa ISACA tawi la
Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Norway inayoshughulikia
maendeleo Afrika Mashariki (Norway Registers Development East Africa
Limited –NRD-) wameandaa semina ya usalama wa matumizi ya kompyuta na
mitandao yake katika nyanja mbalimbali kwa mashirika ya umma, benki,
serikali na watu binafsi.Semina hiyo
inayotarajiwa
kufanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu katika Hoteli ya Nashera mkoani
Morogoro ambapo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe
January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi .
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam Rais wa ISACA Bw.
Boniface Kanemba ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kutokana
na ongezeka la wizi wa mitandao na matumizi mabaya ya mitandao
uliojitokeza katika miaki ya hivi karibuni.
“Mafunzo
haya ni kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka sekta zote za umma na
binafsi pia kutoka nchi zote tano za Afrika Mashariki zikiwemo,
Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kutokana na nchi hizi kuwa na
changamoto sawa na ongezeko la wizi wa mitandao “alisema Kanemba.
Rais huyo
wa ISACA ameongeza kuwa changamoto kubwa ya wizi wa mitandao inatokana
na kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya simu katika kutuma na kupokea
pesa.
Hivi
karibuni, makampuni ya simu yamekuwa yakitumia mtandao mfano M-pesa na
Tigo Pesa kutuma hela kwa wateja ambapo kumekuwa na kesi nyingi za wizi
kwa kutumia miamala hiyo pamoja na upotevu wa nyaraka muhimu
za makampuni binafsi ,umma na Serikali.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa NRD East Afrika Sebastian Marondo akizungumzia
umuhimu wa semina hiyo amesema, “sio jukumu la serikali peka yake
kupambana na uhalifu bali ni jukumu la kila mwananchi ,makampuni na
mashirika binafsi katika kulinda na kujenga nchi yetu.”
ISACA ni
taasisi huru ya kimataifa isiyokuwa ya faida inayohusika katika
kusimamia na kutoa mafunzo na maarifa ya mifumo ya mitandao wakati NRD
East Afrika ni kampuni inayojihusisha na mifumo ya mitandao ya kompyuta
na usalama wake.
No comments:
Post a Comment