Wednesday, August 7, 2013

MAONESHO YA NANE NANE ARUSHA: TAZAMA PICHA NA MAELEZO UMFAHAMU MTANZANIA ALIYETENGENEZA TRECTOR.

  Picha ya juu ni trector iliyotengenezwa na mkulima mbunifu wa Meru-Arusha anayefahamika kwa jina la Justin Mungure. trector hii ameipa jina la "LUKUA-SI" ambapo maana yake ni chimbua ardhi. Trector hii aliitengeneza kwenye karakana yake mwaka 2012 kwa kutumia engine ya pikipiki yenye 125cc. Trector hii ina uwezo wakulima hekari tatu kwa siku ambapo hutumia kiasi cha lita tatu tu za mafuta ya petrol kwa heka moja. Mgunduzi huyu ameshaifanyia trector hii utafiti wa miezi mitano na imeonyesha ufanisi mkubwa kwa wakulima wadogowadogo. "Niliamua kubuni na kutengeneza trector hii inayotumia engine ya pikipiki baada ya kuona kuwa mkulima mdogo hana mtu anayemjali. Kazi ya kulima na kuzalisha mazao ni ngumu japo ni muhimu" alisema Justin Mungure. Pia aliendelea kusisitiza kuwa anaomba serikali iwathamini wagunduzi wa ndani na kuwawezesha ili waweze kufikia malengo yao maana anaamini wapo watanzania wenye uwezo mkubwa sana wa kubuni na kutengeneza vitu mbalimbali na vyenye kuweza kuleta faida kubwa kwa taifa kama walivyo wagunduzi wengine wa nje ya nchi. kwa mawasiliano ya mgunduzi huyu 0754 842 219
  
Maonesho ya nane nane yameanza tarehe 1/08/2013 na yataendelea hadi tarehe 10/08/2013. Lengo la maonesho haya ni kuwapa wakulima na wafugaji wa Tanzania fursa ya kuweza kuonesha utaalamu walionao katika kuzalisha bidhaa mbalimbali. Ujumbe wa mwaka huu ni "Zalisha kwa kuzingatia mahitaji ya soko"

No comments: