Thursday, August 1, 2013

Serikali yatiliana Saini na Uingereza utekelezaji Mradi wa International Inspiration

PIX4
Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano kuhusu mradi wa International Inspiration awamu ya pili, baina ya Tanzania na Uingereza. Mradi huu umekuwa ukitekelezwa kwa muda wa miaka miwili sasa hapanchini na unahusisha michezo mashuleni ambapo jumla ya shule 15 zinanufaika na mradi huo. PIX5Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga  na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakiweka saini kwenye mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.Mradi huu unatekelezwa hapa nchini kwa ushirikia
PIX7.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga  na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bibi Dianna Melrose kushoto wakionesha kwa waandishi wa habari hati za makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa International Inspiration baada ya kumaliza zoezi la utiaji wa saini leo jijini Dar es Salaam.
Na: Frank Shija
Serikali imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wahisani na wadau mbambali ambao wameonyesha nia ya kusaidia kuinua sekta ya michezo hapa nchini.Hayo yamebainishwa na....M.M
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutiliana saini ya mkataba ya makubaliano ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa International Inspiration kati ya Serikali ya Tanzania na Uingereza leo jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo Bibi
Sihaba amesema kuwa aanaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuchagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ishirini zinazotekeleza mradi huo na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa wahisani ambao wamedhamiria kusaidia ukuaji wa michezo Tanzania.
“Ninaishukuru sana Serikali ya Uingereza kwa kuona Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache zinazotekeleza mradi huo,tutaendelea kushirikiana nayi lakini pia nitoa rai kwa wadau wengi kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na yeyote anayetaka kusaidia kukuza sekta ya michezo hapa nchini”. Alsema Bibi Sihaba.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya amesema kuwa inatia faraja kushuhudia utiaji saini makubaliano ya utekelezaji  wa shughuli za mradi wa International Inspiration (II) ambao ulianza miaka miwili iliyopita.
Ameongeza kuwa walipoanza utekelezaji wa shughuli za mradi huu kumekuwapo mawazo na mipango mingi ya namna bora zaidi ya kuutekeleza mradi huu kwa ufanisi mkubwa ili kuleta mafanikio katika Sekta ya Michezo kwa nchi yetu hasa kwa kuzingatia malengo mazima ya mradi, ambayo ni kuhamasisha vijana kushiriki katika Michezo ili kuboresha maisha yao.
Naye Balozi wa Uingereza hapa nchini Diana Melrose amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na  Tanzania katika Nyanja mablimbali ikiwemo sekta ya michezo na kusisitiza kuwa mradi huu umefanikiwa kwa kiasi kikubwa hapa nchini Tanzania.
Mradi wa International Inspiration ulianzishwa mwaka na kamati ya Olympic na Paralympic game ambapo unasimamiwa  na British Council chini ya udhamini wa Uk Sports. Mtekelezaji mkuu wa mradi huu hapa nchini ni Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, BC, Wadau mbalimbali (TOC, TPC, Shule za sekondari zilizoshirikishwa (15)

No comments: