TIME IS MONEY
Matatizo
yetu mengi yanatokana na sisi wenyewe. Wenzetu Ulaya na Marekani
wanasema; “Time is Money”. Kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha
kwamba muda ni pesa. Lakini, tafsiri sahihi hapo ni umuhimu wa muda.
Kwamba muda ni kitu cha thamani sana. Na hakika, kwa mwanadamu, jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya jinsi kesho yako itakavyokuwa.
Tumekuwa watu wa kulalamika sana. Na tumemwachia Mungu jukumu la kutukomboa kutoka kwenye umasikini wetu. Hapana, Mungu hausiki na umasikini wako. Jukumu la kwanza la kujikomboa kutoka kwenye umasikini ni lako mwenyewe. Na hakuna njia ya mkato, bali ni kufanya kazi, kufanya kazi na kufanya kazi. Achana na ndoto za kuamka na kuvuna mamilioni. Bila kufanya kazi!

Inakuwaje basi kwa mwanadamu mmoja awe na muda na mwingine asiwe nao?
Kuwa
au kutokuwa na muda inatokana na mipangalio yako ya maisha. Binadamu
unapaswa kuwa na bajeti ya muda wako. Ni jinsi unavyoutumia muda wako.
Jinsi unavyopangilia mambo yako, ratiba zako na mengineyo.
Ukiwa
na utaratibu huo, basi, waweza kabisa kuwa na muda wa kutosha kufanya
mambo mengine mengi uyapendayo ikiwemo mapumziko, kuwa na muda na
familia yako, kuwa na muda wa kujisomea na mengineyo.
Ndio,
lililo muhimu ni kuwa na vipaumbele. Unapoandika orodha ya shughuli
zako za siku, juma, mwezi na hata mwaka, basi weka kipaumbele katika
mambo ambayo ni muhimu zaidi. Hayo yaweke juu kabisa katika orodha yako.
Kipaumbele kinaweza kutokana na umuhimu wako binafsi kwa jambo fulani.
Usiwe
mtu unayesukuma mambo mbele. Mtu mwenye hulka ya kuahirisha mambo.
Linalowezekana kufanyika lifanye. Kauli za ’ hili nalifanya kesho’ au ’
namwachia Mungu,’ ni kauli za mtu aliyekata tamaa kwenye mapambano ya
maisha.
Wahenga
walinena; ’’Linalowezekana leo lisingoje kesho!’’ Hulka ya kusukumia
mbele mambo ina tafsiri moja tu; kuwa unaongeza mzigo wa mambo ya
kufanya. Huna unachokipunguza. Ni mwanzo wa kupatwa na msongo (stress).
Ni mwanzo wa kuchanganyikiwa. Ndipo hapo utamwona mwanadamu mwenzako
akitembea huku akiongea peke yake.
Ni
muhimu pia kuwa na muda na marafiki. Naam, weka bajeti ya muda. Okoa
muda upate muda wa ziada. Na baadhi ya marafiki zako waweza kuwa sababu
ya matumizi mabaya ya muda wako. Ndio, marafiki wengine ni marafiki wa
kukupotezea muda tu. Angalia, ni marafiki wa aina gani ulio nao.
Inasemwa,
ukitaka kumfahamu mtu alivyo, basi, angalia aina ya marafiki zake. Kwa
mfano kama una rafiki ambaye hazingatii muda, hana miadi ya uhakika,
basi, huyo anaweza kuwa mzigo katika suala zima la matumizi ya muda.
Usiwe
mtu mwenye kufuata mkumbo, eti kwa vile wengine hawazingatii muda,
basi, na wewe unajifanya ni mtu usiyejali muda. Hapo utakuwa unajipoteza
mwenyewe. Ni muhimu, hata unapokuwa na marafiki zako, uwe mbele katika
kuhakikisha mnatumia muda wenu vizuri.
Uwe tayari na mipango kichwani hata kabla hujakutana na rafiki au marafiki zako. Kisha mshirikishe rafiki au marafiki zako katika mipango uliyoifikiria kwenye mambo ya kufanya. Na usiwe mtu mwenye kupanga mambo mia moja kwa wakati mmoja. Uwe na mipango miwili au mitatu ya kujadili na wenzako. Kesho ndio uje na mingine.

bahati mbaya kwetu wanadamu, kuwa muda mwingi sana huwa tunaupoteza
kutokana na kutopangilia vizuri mambo yetu. Upo umuhimu kwa mfano wa
kupangilia shughuli zetu kutokana na sehemu za kijiografia.
Kwa mfano, kama una shughuli ambazo zinahitajika kufanyika mjini, hakikisha kwamba unapokwenda mjini, unazikamilisha zote kwa wakati mmoja. Kwanini uende mjini zaidi ya mara nne kwa siku?
Kwa mfano, kama una shughuli ambazo zinahitajika kufanyika mjini, hakikisha kwamba unapokwenda mjini, unazikamilisha zote kwa wakati mmoja. Kwanini uende mjini zaidi ya mara nne kwa siku?
Naam, Mungu hahusiki na umasikini wako. Muda ni mali. Panga bajeti ya muda wako, sasa! Na hili ni Neno La Leo.
Mshambuliaji
wa Manchester United, Danny Welbeck akishangila na Antonio Valencia
(jezi namba 25) baada ya kuifungia timu yake bao la tatu dhidi ya
Wolverhampton Wanderers katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa
kwenye dimba la Molineux mjini Wolverhampton, England leo. Man Utd
wameshinda mabao 5-0, na mabao hayo yamefungwa na J. Evans, A. Valencia,
D. Welbeck na J.Hernandez aliyefunga mawili.
Beki wa Manchester United, Jonny Evans (aliyenyoosha mkono)…
Mshambuliaji wa Manchester United, Danny Welbeck akishangila na Antonio Valencia (jezi namba 25) baada ya kuifungia timu yake bao la tatu dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa kwenye dimba la Molineux mjini Wolverhampton, England leo. Man Utd wameshinda mabao 5-0, na mabao hayo yamefungwa na J. Evans, A. Valencia, D. Welbeck na J.Hernandez aliyefunga mawili.
Beki wa Manchester United, Jonny Evans (aliyenyoosha mkono) akishangilia pamoja na wenzake baada ya kuifungia timu yake bao dhidi ya Wolverhampton Wanderers jana

UCHAGUZI WAENDELEA KUPAMBA MOTO ARUMERU ARUSHA
Msanii
wa TOT anayekwenda kwa jina la Juakali, akihamasisha watu, baada ya
mgombea wa CCM Arumeru Mashariki, Sioi Sumari na Mratibu kampeni za CCM
Mwigulu Nchemba (kulia) kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni
uliofanyika leo Kata ya Kikatiti A Town.
Sioi akikasalimia katoto kwenye…
Msanii
wa TOT anayekwenda kwa jina la Juakali, akihamasisha watu, baada ya
mgombea wa CCM Arumeru Mashariki, Sioi Sumari na Mratibu kampeni za CCM
Mwigulu Nchemba (kulia) kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni
uliofanyika leo Kata ya Kikatiti A Town.
Sioi akikasalimia katoto kwenye mkutano huo.
Mgombea
ubunge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiwasalimia
wapigakura wake, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha
Mikandini jimboni humo. Kulia ni Mratibu wa kampeni za CCM jimboni humo,
Mwigulu Nchemba.
NI CCM TU: Kina mama na kina baba wa kijiji cha Mikandini wakishangilia kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji hicho.
Wazee
wa Kijiji cha Maroroni jimbo la Arumeru Mashariki wakifuatilia kwa
makini hotuba ya mgombea wa CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
kwenye kijiji hicho.
Wananchi
wa Kijiji cha Maroroni wakiwa wameketi kwenye mawe ili kuweza kupata
kwa undani zaidi hotuba ya mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa
kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji hicho.
Msafara wa mgombea wa CCM ulichanja mbuga katika maeneo ya Kata ya Kikatiti kusaka kura jimboni Arumeru Mashariki.
No comments:
Post a Comment