NI KATIBU WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO AKIUTUBIA NA KUTOA WAZO LA KUOMBA MCHANGO KWA AJIRI YA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA UCHANGUZI WA JIMBO LA ARUMERU-ARUSHA
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kimetangaza mkakati wa kuchangisha fedha kutoka kwa wanchama wake ili kufanikisha kampeni zake kwenye uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha.
Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Aprili Mosi unatokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari, kilichotokea mapema mwaka huu.
Maamuzi hayo yalitokana na kikao cha Kamati Kuu cha CHADEMA kilichofanyika kwa siku Mbili mkoani Arusha ambacho kimetoka na maazimio ya kuhakikisha chama hicho kinakusanya fedha kutoka kwa wananchama wake ili kufanikiwa kutwaa jimbo hilo.
Akitangaza maamuzi hayo kwa Waandishi wa habari kwenye makao makuu ya CHADEMA jijini Dar es salaam, Katibu wa Uenezi Taifa wa chama hicho, John Mnyika, alisema mpango wa kampeni zao katika jimbo la Arumeru Mashariki hautategemea fedha za ruzuku bali watawachangisha wanachama wao ili kufikia malengo yao.
Wakati huo huo kamati kuu ya CHADEMA ilitoa maazimio ya kuhakikisha suala la mabadiliko ya katiba linasemwa katika kila mkutano wa hadhara ili kuwapa fursa wananchi wengi kufahamu kwa undani mabadiliko hayo wakati wakielekea kwenye mchakato wa utoaji wa maoni.
Katika uchaguzi huo wa Arumeru Mashariki, CHADEMA, imemsimamisha mgombea wake Joshua Nasar anayetarajiwa kutoa upinzani mkali kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Siyoi Sumari
BAADA YA KUUTUBIA KILICHOFATA NI KUPONGEZANA
.Ni Dr.Willbrod Silaha na Mgombea ubunge jimbo la Arumeru (Joshua Nassari) mara baada ya kumaliza kuutubia wananchi wa Arumeru.
Waweza toa maoni yako kupitia kwenye nafasi ya maoni (comment)
No comments:
Post a Comment