Tuesday, March 20, 2012

Waziri wa Ofisi ya Rais Utawala Bora Mathias Chikawe Azungumza na waandishi Wa Habari Juu ya Haki za Binaadamu Katika Nchi Options Yetu

Waziri wa Ofisi ya Rais Utawala Bora Mathias Chikawe akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari Ofisini kwake Machi 19.2012 kuhusu Haki za Binaadamu katika nchi yetu. Baada ya kuhurudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Geneva –Uswiss hivi karibuni

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiongea na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) kwenye sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad( SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro,
Mke wa Rias na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(kulia) na Mwenyekiti Taifa wa JUWAKITA Mama Shamim Khan kwa pamoja wakifuatilia ratiba katika Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika Chuo cha Kiislam- Morogoro.Maadhimisho hao yameandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) mkoa Morogoro,Machi 18 2012,
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kiwete akisalimiana na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania ( JUWAKITA) Mkoani Morogoro Machi 18.2012 alipohudhuria Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). yalioandaliwa na jumiya hiyo ya JUWAKITA.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (vazi jeupe) akisindikizwa na Mwenyekiti Taifa wa (JUWAKITA) Shamim Khan, (kushoto) ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Halima Dendegu (wapili kutoka kulia) na Katibu Tawala Mkoa Morogoro Mgeni Baruwani baada ya kumaliza sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro.
Wanafunzi wa madrasa wamsikiliza mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akizungumza nao.
Akina mama mbalimbali wakimsikiliza mama Salma Kikwete.
Wanajumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) mkoani Morogoro wakimkaribisha mgeni rasmi Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete hayupo pichani alipowasili kwenye maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18.2012.

Naibu Waziri wa Ujenzi Dr Harrison Mwakyembe akiongea na waandishi wa  habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maendeleo ya  Afya yake nakusema kwamba yeye sasa yuko fiti kiafya, na ameripoti ofisini  rasmi leo hii alipoulizwa maswali kutoka kwa waandishi wa habari  akasema mambo yote anaichia serikali kupitia tume maalumu iliyoundwa  kufutilia suala la ugonjwa wake.

Uzinduzi wa Kamati ya Wazee ya Kituo cha Amali Mwanakwerekwe.

 MKUU wa Kitengo cha Ushoni katika Kituo cha Mafunzo ya Amali cha Mwanakwerekwe,Maryam Sineni (kulia) akitowa maelezo kwa Ujumbe wa Kamati ya Wazee ilipofanya ziara ya kutembelea Vituo vya Amali Unguja baada ya uzinduliwa wa kamati hiyo uliofanyika katika ukumbi wa kituo hicho Mwanakwerekwe.
MKUU wa kitengo cha Useremala katika kituo cha mafunzo ya amali cha Mwanakwerekwe, Mohammed Juma (kushoto) akiwapatia maelezo wajumbe wa kamati ya wazee wa kituo hicho muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa kamati hiyo katika ukumbi  Mwanakwerekwe.

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa Watembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro

 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.
 Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akipokea salaam za kukaribishwa kutoka kwa wanafunzi waaShule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha (kushoto) wakati akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa Mh. Lowassa,Mama Regina Lowassa na wa pili kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo,Sista Dennis.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa(Wa pili Kushoto) akiongea  na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.Kushoto ni  Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Mh. Waziri Mkuu Mstaafu.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.

TANZANIA REPRESENTED AT THE COMMONWEALTH DAY IN LONDON

 Tanzania flag being flown at the Abbey
Her Majesty Queen Elizabeth II 
Mr and Mrs Peter kallaghe arriving for service 
--
By Ayoub  mzee

Commonwealth Day is an opportunity to promote understanding on global issues, international co-operation and the work of the Commonwealth’s organisations, which aim to improve the lives of its citizens.
It is celebrated on the second Monday in March every year.
The theme for Commonwealth Day 2012 is Connecting Cultures
The  observance  is  the  largest  uk  annual  multi faith gathering which  is  always  honoured  by the  presence  of  the head  of  the  commonwealth HER  MAJESTY  QUEEN  ELIZABETH II ,The  Duke of  Edinburgh ,Prince  Charles and  the  duchess  of  Cornwall.Tanzania  was  represented  by  H.E  Peter Kallaghe

Kutoka Zanzibar:Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad Akutana na Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi akifafanua jambo katika mkutano wake na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo,hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar,hii ni baada ya kumaliza kwa Ziara yake ya Kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hio.Kushoto yake ni Waziri wa Habari Umaduni Utalii na Michezo Zanzibar Abdillah Jihad Hassan.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Michezo na Utamaduni Othman Mohd (Makombora)akifafanua jambo katika Mkutano wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,uliofanyika hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Mjini Zanzibar.
Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shairif Hamadi alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo,hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar,hii ni baada ya kumaliza kwa Ziara yake ya Kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hio.
Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shairif Hamadi alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo,hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar,hii ni baada ya kumaliza kwa Ziara yake ya Kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hio.

YOUNG D, GODZILLA WALIVYOKAMUA NDANI YA DAR LIVE{VIDEO}




Wasanii Wa Music Academy Wakamua Dar Live

Rapa wa Academy Rahim akifanya makamuzi.
 
Mwalimu(Hamza Kalala) akiwapa tafu kupiga gitaa la solo ndani ya dar live.
Paul Mwanja mpiga drum wa academy akiwa mzigoni.
Sebene kwa kwenda mbele.
Wana Academia wakiimba wimbo wao mpya unaoitwa linda.JPG
---
Saalam,

Baada ya kufanikisha uundwaji wa Music Academy Tanzania chini ya usimamizi wa ASET na URBAN PULSE CREATIVE kwa mara ya kwanza wana academia walipata fursa ya kutumbuiza live stejini katika ukumbi mpya wa kisasa Dar Live uliopo mbagala siku ya  jumamosi tarehe 17.3.2012

Hii ilikuwa ni mojawapo ya hatua waliopiga kuonyesha vipaji vyao na kuwajengea uzoefu kutumbuiza mbele za maelfu ya mashabiki waliojitokeza kupata burudani.

Music Academy inaendelea kutoa mafunzo na pia kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.



IKULU:Rais Jakaya Kikwete Amwapisha Meja Jenerali Samwel Ndomba Kuwa Mkuu Mpya wa JKT

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,(kushoto)Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha mkuu huyo mpya wa JKT ikulu jijini Dar es Salaam leo
Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.
Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndomba wakati wa hafla ya kumuapisha iliyofanyika leo asubuhi ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mzee Albert Ndomba(85),baba mzazi wa Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba(wapili kushoto) baada ya halfa ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni mke wa Meja Jenerali Ndomba na waliosimama nyuma ni wanafamilia.
Amiri Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Picha na Freddy Maro-IKULU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan Akutana na Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Nchini Tanzania

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan akizumgumza na Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Nchini Tanzania Bw Greyson Lazaro Mlanga walipokwenda kumuona Ofisini kweke Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu Hassan alipokuwa na  Mazungumzo na Viongozi wa chama cha  walemavu wasiooma Nchini Tanzania wakati walipomtembelea Ofisini Kwake Mtaa wa Luthuli Mjini Dar es Salaam.Picha na Ali Meja

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungmza na Viongozi wa CCM WA Mkoa wa Kaskazini Pemba Kwenye Ukumbi wa Skuli ya Micheweni Pemba.Kushoto yake ni Mwenyekiti wa CC Mkoa wa Kaskazini Pemba Nd. Mberwa Hamad Mberwa, kulia yake ni Mjumbe wa Kamatiya Siasa ya Mkoa huo Mh. Dadi Faki Dadi na Pembeni yake ni Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleiman Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi mchango wa Shilingi 1,000,000/- kwa Mwalimu wa Madrasatul Jabal Hira ya Utaani Wete Ustaadhi Khamis Hamad Faki kwa ajili ya kusadia uendelezaji wa Madrasa hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Baadhi ya Viongozi wa Madrasatul Jabal Hira ya Utaani Wete Pemba ambapo alikuwa Mgeni rasmi katika Maulidi ya Chuo hicho kutukuza Uzawa wa Mtume Muhammad { SAW }.
Waumini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Mtume Muhammad { SAW } katika hafla ya Maulidi ya Uzawa wa Kiongozi huyo iliyoandaliwa na Madrasatul Jabal Hira iliyopo Mtaa WA Utaani Wete Pemba ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia kazi za mikono zinazoendeshwa na Kikundi cha Ushirika cha Tuvumiliane Women Group kiliopo Mjini Wete akiwa pamoja na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi. Balozi Seif alihamasika kuchangia shilingi 500,000/- wakati Mama Asha akachangia shilingi 300,000/- kuuendeleza Ushirika huo.
Katibu wa Ushirika wa Ufugaji Samaki wa Kishakaashishangi wa Kiuyu Minungwini Nd. Othman Bakari akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ai Iddi jinsi ya harakati za Mradi wao ulioanzishwa mwaka 1994.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kikagua Maendeleo ya Ujenzi wa Tuta la kuzuia Maji ya Bahari yasivamie mashamba ya Kilimo cha Mpunga katika Bonde la Mziwanda Wilaya ya Micheweni

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa Atunukiwa Tuzo na Mfuko wa Bima ya Afya

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa Tuzo ya Kuenzi mchango wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Bima ya Afya katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo uziliofanyika kwenye ofisi kuu ya mfuko, barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Machi 19, 2012.Kushoto ni Waziri Mkuu, Frederick Sumaye ambaye pia alipewe tuzo hiyo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa (katikati) na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Bima ya Afya kwenye ofisi kuu ya mfuko huo barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam Machi 19, 2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments: