Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini.
Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili.Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.
Awali, Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.
No comments:
Post a Comment