Monday, April 23, 2012

'LAIVU" VURUGU CHUO CHA MKWAWA ZAENDELEA FFU NUSURU WACHEZEE KICHAPO

Askari wa FFU Iringa akiwatuliza wanafunzi wa chuo cha Mkwawa Iringa wasilipige mawe gari la msajili wa Mahakama kanda ya Iringa kwa madai halihusiki
Hapa askari zaidi wakiruka katika gari hilo ili kunusuru maisha ya dereva na msajili baada ya kuvamiwa na wanafunzi hao wakati akitoka maeneo ya Pawaga
Wanafunzi na wananchi wakiwa wamezunguka gari la msajili wa Mahakama kanda ya Iringa Philimon Matogoro
hapa wakishangilia baada ya askari kuondoka eneo la tukio
Gari la Msajili wa mahakama kanda ya Iringa likiwa limezuiwa
Kijana wa CCM akimwokoa diwani Kikulacho baada ya jitihada za kuwaomba wanafunzi hao wasifanye fujo kugonga mwamba
Diwani Kikulacho akijiandaa kutimua mbio baada ya wanafunzi kuchachamaa
Diwani akiokolewa asichezee kichapo
Vurugu za kutaka wakala wa barabara mkoa wa Iringa (TANROADs) kuweka matuta katika lango la chuo cha elimu Mkwawa Iringa bado zinaendelea huku diwani wa kata hiyo ya Mkwawa Thoabias Kikula na askari wa FFU waliokuwa katika gari la msajili wa Mahakama kanda ya Iringa wakifanyiwa vurugu kwa kutaka kuchezea kichapo wao na dereva .

Diwani Kikula ambaye kwa sasa ameokolewa kutoka eneo hilo la vijana wa CCM ili kunusuru kuchezea kichapo ameunga na askari polisi walikuwepo eneo hilo kwenda kwa mkuu wa chuo hicho ili kuangalia uwezekano wa kwenda TANROADs .Wakati diwani huyo akiokolewa eneo hilo wanafunzi hao na wananchi wa eneo hilo wameanza kutafuta majembe ili kuchimba barabara hiyo .

No comments: