Monday, April 23, 2012

SIMBA YAICHAPA MORO UNITED MAGOLI 3-0 UWANJA WA TAIFA

Aonesha unyama wake leo

 Mchezaji wa timu ya Moro United Eric Mawala akijaribu kuokoa mpira, huku mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akimkaba katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jioni hii jijini Dar es salaam, ambapo Simba imeibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya Moro United, kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 59.
Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Haruna Moshi, Patrick Mafisanga pamoja na Mchezaji Felix Sunzu kutoka nchini Zambia.
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kufanya vizuri na katika mchezo wao na timu ya Moro United.

No comments: