Wednesday, April 18, 2012

KAZI KWA WANAKAGERA LEO WAMEPOKE ZANA

MKOA WA KAGERA WAPATA USAFIRI NA VIFAA VYA KUKUSANYIA TAKWIMU ZA KILIMO VIJIJINI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera (katikati) akitoa neno la shukrani na kuwaasa wakurugenzi  wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kuzitumia Pikipiki hizo kwa Kusudi lililokusudiwa.
Mkuu wa Mkoa akimshukuru Bi. Akasaka Kyoko Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Japani (JICA) kwa ufadhili wa Pikipiki za kukusanya Takwimu za Kilimo vijijini.
Pikipiki Nane ambazo zimetolewa kwa Mkoa wa Kagera kutoka Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na JICA kutoka nchini Japani

Picha/Habari: Sylvester Raphael, Afisa Habari Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akabidhi pikipiki nane kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali za kilimo kutoka  vijijini katika Mkoa wa Kagera.

Pikipiki hizo zimetolewa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikishirikiana na shiririka la Kimataifala Uhusiano la nchini Japan (Japan International Cooperation Agency, (JICA)   ambalo limewakilishwa na Bi. Akasaka Kyoko wakati wa kukabidhi  pikipiki hizo nane.

Mhe.  Massawe pia amewasistiza sana Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa kutunza pikipiki hizo na kuzifanyia kazi iliyokusudiwa na si vinginevyo. Aidha aliwaomba maafisa kilimo watakaozitumia pikipiki hizo kukusanya takwimu za kweli ili kuondokana na tatizo  takwimu zisizo sahihi.

Pamoja na pikipiki hizo na JICA pia waliendesha mafunzo ya ukusanyaji takwimu na kugawa kompyuta moja na mfuko wake, na Flashi mojamoja kwa kila Halmashauri ya wilaya na manispaa kwa ajili ya kukusanya na kutunza takwimu za kilimo vijijini.

Mkuu wa Mkoa aliwashukuru JICA kwa kujitolea kuleta maendeleo Tanzania na hasa katika mkoa wa Kagera. Ambapo pia amewahakikishia JICA kuwa serikali itaendelea kuhamasisha wananchi kuondokana na kilimo cha kuchumia tumbo na kujikimu na kuhamia katika kilimo cha biashara zaidi.

No comments: