Wednesday, April 18, 2012

TADHIMINI YA GHARAMA ZILIZOTUMIKA KATIKA KUMALIZA MSIBA WA KANUMBA

 MAGAZETI YA LEO; MSIBA WA KANUMBA MIL. 70 ZATUMIKA

WAKATI kamati ya Mazishi ya msanii wa Filamu nchini  Steven Kanumba ikikanusha kuwepo ubadhirifu Fedha za Mapato na Matumizi zilizokusanywa tangu kifo cha msanii huyo, leo imeanika mchanganuo wa Mapato na Matumizi ya fedha zilizokusanywa. 

Mwenyekiti wa Kamati Hiyo Gabriel Mtitu amewaambia waandishi wa Habari jijini Dar es salaam jumla ya shilingi mil.52,352,000 tu ndizo zilikusanywa.

Alisema katika fedha hizo zilizopatikana zilitumika shilingi milioni 52,102,000, hivyo kubaki shingi milioni nne tu ambazo tayari amekabidhiwa mama mzazi wa marehemu.

Aidha Mtitu amesema pesa zilizopatikana kwenye M Pesa ni shilingi 300,000 wakati kwenye Tigo Pesa ni shilingi 150,000. 

Katika hatua nyingine Mtitu ametoa shukrani kwa wale wote ambao wameweza kutoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha msiba huo.

No comments: