Saturday, April 7, 2012

KIFO CHA MWIGIZAJI KANUMBA

 
Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, FOUR WAYS BUKOBA itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.

Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
Hapo chini ni baadhi ya kauli nilizokutana nazo kwenye facebook wakati huu na chini yake ni maneno ya mwisho STEVEN KANUMBA kuyaandika kwenye kurasa zake za facebook na twitter

No comments: