Askari wa Kikosi cha kuzima moto jijini Arusha wakijaribu kuzima moto huo bila mafanikio.
PICHA NA MWIJA MUSHI WA FOUR WAYS BUKOBA- ARUSHA
Moshi mkubwa ukiwa umetanda angani kutokana na moto huo.
Umati wa watu ukisangalia moto aliokuwa ukiunguza maduka jijini Arusha leo.
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-ARUSHA
WANANACHI wa jiji la Arusha wameomba serikali kuongeza zaidi vifaa kwa kikosi cha zima moto ijini hapa kwa kuwa mara nyingi sana kikosi hicho kinashindwa kuokoa wananchi katika majanga ya moto kutokana na kutokuwa na vifaa vya kutosha yakiwemo maji
Wakizungumza na Waandishi wa habari jijii hapa katika tukio la kuungua kwa maduka tisa yaliyopo Stendi ya mkoa katika mtaa wa majengo wananchi hao walisema ukosefu wa maji ya kutosha kwa kikosi hicho unachanmgia sana maafa na kwa hali hiyo Serikali inatakiwa kuliangalia hilo
Walisema kuwa mara nyingi sana kikosi hicho cha kuzima moto kinafima kwa ajili ya kuokoa bidhaa pamoja na maisha ya watu ambao wamenusurika na ajali za moto lakini wanashindwa kufanya kazi zao
Wananchi hao walifafanua kuwa endapo Kama hali hiyo ya uzembe itaendelea basi kikosi hicho kitakuwa hakina faida kwa wananchi, na hali hiyo inatakiwa kudhibitiwa mara moja kwa ajili ya kuokoa maafa ya ajali za moto
Walisema kuwa katika tukio hilo la kungua kwa maduka kama tisa ya biashara mbalimbali ambalo lilitokea majira ya saa tisa za mchana katika mtaa wa majengo stendi kubwa walisema kuwa magari yaliokuwa na maji yalifika kwa muda muafaka lakini hawakuwa na maji ya kutosha
Wananchi hao walisema kuwa iwapo kama Magari hayo ya Fire yangekuwa na maji ya kutosha basi ni wazi kuwa kwa kiwango kikubwa sana wangeweza kuokoa maduka hayo dhidi ya moto mkubwa
Katika hatua nyingine Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Bw Akili Mpwapwa alibitisha kuungua kwa maduka hayo tisa na kusema kuwa chanzo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment