Kutoka Facebook: " Walitoka Kwetu, Lakini, Hawakuwa Wa Kwetu"- Yohana 2:11
"Kwa uongozi wa vyama vyote vya siasa aidha na vilabu vya mpira muonapo mnakimbiwa na wanachama wenu au wanawahama. Take it positively that mnaonyeshwa kuwa hao wanaoondoka si wenzenu au wa kwenu. La sivyo wasingelifanya hivyo. Sibwabwaji bali someni 1 Yohana 2:19 ambapo imeandikwa "Walitoka kwetu lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu wangalikaa na kubakia pamoja nasi. Lakini wametoka ili wafunuliwe kwamba sio wote walio wa kwetu". Namaanisha nini? Namaanisha hivi, fulani (jina naminya) ametoka CCM /CDM kwa sababu hakuwa wa CCM/CDM. Kwa sababu kama angekuwa ni wa vyama hivyo, angeendelea kubakia mle ije mvua ije jua. Kwa hio kuondoka kwake wanaashiriwa waliobakia kuwa hao tangu awali hawakuwa wa vyama hivyo kiitikadi. Sio hivyo pia bado watakuwepo wengine watakaotoka!
Kuna kila dalili very soon and not even in a distant future there will be a migration of politicians moving from one party to another! Why kwa sababu wanatafuta nafasi ya ubunge au udiwani . It is obvious kama niko CCM na nina kiu ya kutafuta ubunge kwenye jimbo X. Lakini najua kwa mujibu wa kura ya maoni siwezi kumngoa mbunge wa sasa kwa kupitia CCM. Hekima inanituma nihamie chama kingine wakati huu ili iwe rahisi come 2015 kwa sababu wapiga kura huenda wakanipa. Hapo hakuna anaeongozwa na itikadi yachama bali itikadi ya ubinafsi. Japo nikiulizwa nitasema nimeombwa na wananchi walio wengi nigombee! Unless Katiba ijayo itaruhusu wagombea binafsi!"- Tsere
No comments:
Post a Comment