Wednesday, April 11, 2012

LULU KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO



M
SANII Elizabeth Michael (Lulu), ameiambia polisi kuwa kifo cha Steven Kanumba kimetokana na ugomvi kati yao, huku taarifa nyingine zikieleza kuwa huenda Lulu akafikishwa mahakamani leo.
Habari zilizopatikana jana kutoka Kituo cha Polisi Oysterbay zilieleza kuwa, Lulu alisema kuwa kulitokea ugomvi kati yake na Kanumba baada yeye kuzungumza na simu kutoka kwa mtu maarufu anayetajwa kuwa mpenzi wake.
Kanumba akamfokea na ndiyo ugomvi ukaanzia hapo," chanzo hicho kimesema.
"Lulu alisema kuwa ugomvi ulitokana na simu aliyopigiwa na mpenzi wake mwingine, ambaye ni mtu maarufu nchini, ndipo
Chanzo hicho kiliongeza kuwa baada ya Kanumba kuanguka, Lulu alitoka nje na kuondoka kwa gari lake hadi maeneo ya Coco Beach, lakini baadaye daktari wa Kanumba alimpigia simu akimtaka arudi ili wampeleke hospitali.
Chanzo kiliongeza kuwa tangu Lulu alipofikishwa kituoni hapo amekuwa mtulivu asiye na wasiwasi wowote hata katika mahojiano na polisi.
Katika hatua nyingine, Polisi wa kituo hicho jana walipata wakati mgumu baada ya kuibuka kundi la vijana waliotokea makaburi ya Kinondoni kumzika Kanumba, walioandamana wakidai wanamtaka Lulu.
Hata hivyo vijana hao walitawanyika baada ya kuona askari wakiwa tayari kupambana nao na kukimbia maeneo mbalimbali.
Katika hatua nyingine Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa, 
Msanii Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu huenda akafikishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kuhusika na kifo cha Steven Kanumba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela aliliambia gazeti hili jana kuwa Lulu atafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mara baada ya polisi kupata ripoti ya vipimo kutoka Mkemea mkuu wa Serikali.
Aliongeza ripoti hiyo itaweza kuwasaidia kuandika mashtaka ili yaweze kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya kumfikisha mahakamani. 
Kamanda Kenyela alisema kuwa, ripoti ya madaktari imewasilishwa juzi na kwamba imeonyesha kuwa Kanumba amefariki kwa ugonjwa wa mtikisiko wa ubongo.
Chanzo:Mwananchi

No comments: