Monday, April 9, 2012

TUMEFIKA SALAMA MJINI DODOMA TAYARI KWA KUMUVUZISHA MATUKIO


Tunamshukuru Mungu tumefika salama mjini Dodoma tukiwa na mwanablogu mwenzangu Michuzi Junior, ambapo leo tutakuwa tukimuvuzisha moja kwa moja matukio ya Tamasha la Pasaka kwenye uwanja wa Jamhuri kuanzia mcahana huu. 
Safari ilikuwa ni nzuri na dereva tuliyesafiri naye katika basi la kampuni ya Al-Saeedy ni dereva aliyefundishwa akafundishika na anajua kuitumia barabara vyema, kwani haonyeshi kuwa mtu mwenye papara barabarani, laiti  kama madereva wengi  wangekuwa hivyo nadhani tungepunguza sana ajali za babarani, kwani ni dereva anayejua udereva wa kujihami, asante mungu kwa kumuongoza vyema.

Lakini pia barabarani hakukosi matukio katika picha hapo juu  ni Gairo mkoani Morogoro  wananchi wakijadili mambo mbalimbali kuhusu maisha na kazi zao za kila siku kandokando ya barabara, huku watoto wao wakiwa wamekaa chini huku wamejifunika ngua kujikinga na jua kali la mchana, japokuwa wao wanajisikia kwamba jua ni kali sana, lakini mimi hali hii nimeifurahia sana kwani jua ni kali lakini kuna kibaridi kwa mbali. tofauti na jiji la  Dar es salaam ambako jua ni kali lakini pia unakumbana na joto kali ukichanganya vyote utajuta kuzaliwa

No comments: