Thursday, May 31, 2012

Benki Ya Wakulima Kuanza



SERIKALI imesema kuwa Benki ya Wakulima inatarajiwa kukamilika wakati wowote mwaka huu na kuanza kutoa mikopo mikubwa na ya muda mrefu ili kuboresha sekta ya kilimo nchini iliyo tegemeo kubwa katika kutoa ajira na kuongeza kipato cha wananchi wengi.

Aidha, serikali pia imekubali kuongeza mtaji kwenye Benki ya Rasilimali nchini (TIB) ili kuiwezesha kuwa na uwezo wa kutoa fedha zitakazotumika kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, ikiwemo ya uboreshaji wa miundombinu.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene mara baada ya kufungua mkutano mkuu wa 38 wa Taasisi za Benki za Maendeleo barani Afrika (AADFI) unaofanyika jijini hapa chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIB, Peter Noni.

Mbene alisema kuwa, serikali imekubali kutenga kati ya dola za Marekani milioni 400 na 500 kwa ajili hiyo ambapo benki hiyo ya wakulima inatarajiwa...Somba zaidi http://www.freemedia.co.tz

No comments: