Friday, May 11, 2012

Kamanda Faustine Shilogile wa ilala awataka wananchi kupambana na dawa za kulevya




NA MWANDISHI WETU

  KAMANDA wa Kipolisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile amesema suala la kupambana na dawa za kulevya ni mtambuka hivyo ni wakati kwa kila mwanajamii kujitokeza katika kupambana na tatizo hilo.

  Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumza na Fullshangweblog kuhusu kuibuka kwa vikundi vya vijana wanaojihusisha na uvutaji wa dawa hizo.

  Alisema wananchi wanapaswa kuondokana na mawazo kuwa mapambano ya udhibiti wa uingizwaji wa mihadarati nchini  yanalihusu jeshi la polisi pekee bali mapambano hayo yanazihusu Wizara ya Kazi na Ajira, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  Shilogile alisema iwapo Wizara hizo, zitawajibika ipasavyo kwa kuyaunganisha makundi ya vijana ambao wengi wao ndiyo waathirika wa kubwa wa matumizi ya dawa za kulevya katika shrikisha katika miradi ikiwa ni pamoja kuwaanzishia mashindano mbalimbali ya michezo.

“Unajua vijana wengi wa Tanzania wamekuwa hawana ajira kutokutokana na hali hiyo hujikuta muda mwingi wakiwa hawana la kufanya mwisho wasiku hujikuta wakitumiwa na baadhi ya matajiri kuwauzia dawa hizo na hatimaye kuwa watumiaji hadi kuathirika na kupoteza uwezo wa kufanya kazi hivyo kulifanya taifa kupoteza nguvu kazi”alisema Shilogile. 
Shilogile alisema wamekuwa wakijaribu mbinu mbalimbali hata kutumia michezo kwa lengo la kuwashuhulisha vijana hao ili wasipate muda wa kuwaza mabo mbaya kama hayo.

  Alitanabaisha kuwa kuna mashindano ambayo ameanzishwa na Makanda na baadhi ya mikoa ikiwa ni moja ya kampeni ya kuwaweka vijana katika mazingira kuondokana na msongo wa mawazo wa ukosefu wa ajira ambao huwa unawasukuma katika kujiingiza kwenye uhalifu.


Hata hivyo, Shilogile alisema wamekuwa wakifanya opereshini mbalimbali za kuwakamata wauzaji wa kati ambapo hadi sasa kuna baadhi wamekwisha wafungulia kesi mahakamani.
 

No comments: